Mheshimiwa Augustine Phillip Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akilakiwa na mwenyeji wake Mheshimiwa Kang Kyung-hwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa mazungumzo ya kikazi tarehe 31 Januari 2018.
Mheshimiwa Augustine Mahiga na mwenyeji wake Mheshimiwa Kang Kyung-hwa wakiwa kwenye mazungumzo ya kikazi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Korea tarehe 31 Januari 2018. Wakwanza kushoto ni Mheshimiwa Matilda Masuka, Balozi wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Korea. Wakwanza kulia ni Bw. Park Young min, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Korea.
Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya picha ya mlima
Kilimanjaro na kinyago cha mnyama waziri mwenzake wa Jamhuri ya Korea
Mheshimiwa Kang Kyung-hwa baada ya kukamilisha mazungumzo ya kikazi
yanayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na uchumi baina ya nchi
hizo mbili.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Korea wakiwa kwenye picha
ya pamoja baada ya kukamilisha mazungumzo ya kikazi. Wakwanza kulia ni
Mheshimiwa Balozi Matilda Masuka, Balozi wa Tanzania nchini Korea
Kusini, Bi. Bertha Makilagi, afisa dawati wa Korea Kusini, Wizara ya
Mambo ya Nje, Bw. Park Young min, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afrika,
Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment