Pages

Thursday, February 1, 2018

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wapewa Mafunzo na kampuni ya Medtronic ya Mfumo wa Umeme wa Moyo (Electrocardiogram – ECG)


Picha no. 1
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwtete (JKCI) Peter Kisenge na Prof. Ahmed Osman wa Broward General Medical Centre ya nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua na kumuwekea kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri  (pace maker) ikiwa ni sehemu ya  mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa na  kampuni ya Medtronic  tawi la  Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
picha no. 3
Prof. Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo ya mfumo wa umeme wa Moyo (ElectrocardiogramECG)  kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo yaliyoandaliwa na  kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
picha no. 4
Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa  kampuni ya Medtronic ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo wakati wa  mafunzo ya mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram – ECG) kwa wafanyakazi wa JKCI yaliyoandaliwa na kampuni hiyo.
picha no. 5
Prof. Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi  mfumo wa umeme wa Moyo (ElectrocardiogramECG)  unavyofanya kazi mwilini wakati wa mafunzo hayo yanayoenda sambamba na vitendo  ya siku tano   yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
picha no. 6 picha no. 7
Wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Prof. Ahmed Osman (hayupo pichani)  kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha jinsi  mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram -ECG)  unavyofanya kazi mwilini.
Picha na JKCI

No comments:

Post a Comment