Madaktari Bingwa wa magonjwa ya
Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)na wenzao wa
Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia
wakifanya upasuaji kwa mtoto ambaye vyumba vyake vya moyo
havijakamilika na hivyo damu kwenda kwa wingi kwenye mapafu katika kambi
ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo.
Picha na JKCI
Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa
Moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye
moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) katika kambi maalum ya
siku tano ya matibabu ya moyo iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo.
Jumla ya wagonjwa 16 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea
vizuri kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima saba.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Open
Heart International ya nchini Australia Russel Lee akiongea na waandishi
wa Habari kuhusu upasuaji wa moyo wa mtoto ambao umekaa upande wa kulia
na mishipa yake ya damu chafu na safi imeingiliana katika upasuaji huo
wameweza kulinda mapafu yalikuwa yanapokea damu kwa wingi kutoka
kwenye mishipa ya moyo na mtoto kawekewa kifaa ambacho kitamsaidia moyo
wake kufanya kazi vizuri (Pace Maker). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau.
No comments:
Post a Comment