Shirika
la Kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa gari aina ya Toyota
Landcruiser katika Halmashauri ya Mji Kahama mkoa wa Shinyanga kwa
ajili ya kusaidia ufuatiliaji wa matukio ya ukatili na unyanyasaji wa
watoto.
Mbali
na kukabidhi gari hilo,Save The Children pia imekabidhi pikipiki mbili
aina ya Boxer,Kompyuta mpakato moja (Laptop) na Ipad moja kwa shirika la
KIWOHEDE linalotekeleza mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi
kwa watoto katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Hafla fupi ya makabidhiano hayo
imefanyika leo Ijumaa,Desemba Mosi,2017 katika viwanja vya Halmashauri
ya Kahama Mji wilayani Kahama,mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi,gari,pikipiki,laptop na Ipad, Meneja wa Shirika la Save The
Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema vifaa hivyo vitasaidia
katika utendaji kazi kupambana na ukatili dhidi ya watoto.
“Leo ni siku ya Ukimwi duniani
na sisi tumeona tushiriki katika siku hii ili kuonesha kwamba ukatili ni
njia mojawapo ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Mradi wetu umeisha
lakini mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto yanaendelea, kwa hiyo
tunakabidhi gari hili ili mapambano yaendelee”,alisema Malima.
“Vifaa hivi likiwemo gari hili
vitakwenda kufanya kazi za mapambano dhidi ya ukatili wa watoto,tunaomba
likafanye kazi kama ilivyokusudiwa ili kuhakikisha kuwa vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto vinaisha mkoani Shinyanga”,aliongeza Malima.
Aidha alisema tangu mwaka 2014
walikuwa wanatekeleza mradi wa Ukatili dhidi ya watotokatika halmashauri
ya Mji Kahama,Manispaa ya Shinyanga na Shinyanga Vijijini na baada ya
mradi kuisha mwaka huu wametoa gari hilo kwa halmashauri ya Kahama Mji
kwani imekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya ukatili dhidi ya
watoto.
“Tunawapongeza sana halmashauri
ya Kahama Mji kwa kuwa mfano mzuri katika vita dhidi ya ukatili wa
kijinsia na watoto,wameonesha hatua za ziada,waliamua kuubeba mradi huu
na kuufanya wao,tunaamini wataendeleza mapambano”,alisema Malima.
Hata hivyo,Kaimu Mkurugenzi wa
halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela aliuhakikishia uongozi wa shirika
hilo kuwa watalitunza na kulitumia gari hilo kwa malengo
yaliyokusudiwa.
“Mradi wa wenzetu Save the
Chidren kuisha muda wake, wamekabidhi vifaa hivi ili shughuli za
mapambano ya ukatili dhidi ya watoto ziendelee”,alisema.
“Baada ya mradi kuisha,ili
shughuli zilizokuwa zinatekelezwa ziweze kuendelea,utaratibu huwa ni
lazima mashirika husika yaendelee kuona namna ya kujenga uwezo kwenye
taasisi ambazo walikuwa wanafanya nazo kazi ili shughuli zilizokuwa
zimeanzishwa ziweze kuendelezwa”,alifafanua Kwela.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa
halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija alilishukuru shirika hilo kwa
ushirikiano ambao limekuwa likiwapa na kuongeza kuwa suala la ukatili
dhidi ya watoto linapaswa kufanywa kwa vitendo kama vile Save the
Children walivyoonesha kwa kutoa vifaa hivyo vya kutendea kazi.
Naye Mratibu wa Mradi wa
kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE,
Lulu Makwale alilishukuru shirika la Save the Children kwa kuwapatia
msaada wa pikipiki mbili,laptop na Ipad vifaa ambavyo vitasaidia katika
utekelezaji wa mradi huo katika Halmashauri ya Ushetu.
Makabidhiano hayo pia
yalishuhudiwa na Katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela
alilishukuru shirika hilo kwa msaada wa gari na kuongeza kuwa litasaidia
katika kupunguza changamoto ya usafiri katika halmashauri hiyo.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI WAKATI WA MAKABIDHIANO HAYO
Meneja wa Shirika la Save The
Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati akikabidhi
gari katika halmashauri ya Kahama Mji na pikipiki,laptop na Ipad kwa
shirika la KIWOHEDE leo katika viwanja vya Kahama Mji,wilayani Kahama.Wa
kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija.
Kulia ni Mratibu wa ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala shirika la
Save The Children,Alex Enock akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa
halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela.Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Gari na pikipiki zilizotolewa na shirika la Save The Chilren vikiwa nje ya ofisi za halmashauri ya Kahama Mji.
Meneja wa Shirika la Save The
Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima (kulia) akimkabidhi funguo za
gari Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija.
Katikati ni Mwenyekiti wa
halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija akionesha funguo za gari
lililotolewa na shirika la Save the Children kwa ajili ya kuendeleza
mapambano dhidi ya ukatili wa watoto.
Mwenyekiti wa halmashauri ya
Kahama Mji,Abel Shija akiwa ndani ya gari.Mwingine aliyemo ndani ya gari
ni Mratibu wa mradi wa afya ya uzazi na jinsia na mradi wa kupambana na
mila na desturi kandamizi kwa watoto kutoka Save the Children, John
Komba (kulia).
Meneja wa Shirika la Save The
Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akionesha funguo za pikipiki
kabla ya kukabidhi pikipiki hizo kwa Mratibu wa Mradi wa kupambana na
mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE, Lulu Makwale
(kulia).
Meneja wa Shirika la Save The
Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akikabidhi laptop kwa Mratibu
wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la
KIWOHEDE, Lulu Makwale (kulia).
Meneja wa Shirika la Save The
Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akikabidhi Ipad kwa Mratibu wa
Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la
KIWOHEDE, Lulu Makwale (kulia).
Mratibu wa Mradi wa kupambana
na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE , Lulu
Makwale akionesha Ipad na funguo za pikipiki.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija
akimkabidhi Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,
Benety Malima, cheti cha kutambua kazi nzuri zilizofanywa na shirika
hilo kwenye halmashauri ya Kahama Mji hususani katika mapambano dhidi ya
ukatili wa watoto.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,
Benety Malima akionesha cheti kilichotolewa na halmashauri ya Kahama Mji
kutambua kazi za shirika la Save The Children.
Mratibu wa ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala
shirika la Save The Children,Alex Enock akiwa ameshikilia cheti
hicho.Katikati ni Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa
Shinyanga, Benety Malima.Kulia ni Mratibu wa mradi wa afya ya uzazi na
jinsia na mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto
kutoka Save the Chilren, John Komba.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment