Mfumo wa Kukusanya Mapato
Kielekroniki (eRCS) umeonyesha mafanikio makubwa kwa miezi mitatu ya
mwanzo ya Julai, Agosti na Septemba 2017, baada ya Makusanyo ya Kodi kwa
Upande wa Zanzibar (ZRB) kupitia eRCS kufikia Shilingi Bilioni.7.2,
ukilinganisha na Shilingi Bilioni 3.5, ZRB walizokusanya kipindi Kama
hicho mwaka 2016 kabla ya mfumo wa eRCS.
Makusanyo hayo yakiwa ni Ongezeko
la Shilingi Bilioni 3.6 sawasawa na asilimia102%. Ni zaidi ya Mara
mbili ya makusanyo ya mwaka Jana kabla ya mfumo wa eRCS, yanayofikia
shilingi Bilioni 7.2 ni majumuisho wa Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty) na
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Baada ya kukata Marejesho.
Wakati huo huo Taarifa tulizonazo
kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni kwamba makusanyo ya kodi
yanayotokana na kampuni za simu, kwa kutumia eRCS TRA wamefanikiwa
kuongeza makusanyo kwa asilimia 21% kwa kukusanya Jumla ya shilingi
Bilioni 128.9 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba
2017, ukilinganisha na makusanyo ya miezi ya Aprili, Mei na Juni 2017
kabla ya kuanza kutumia mfumo wa eRCS.
Aprili, Mei na Juni 2017 kabla ya eRCS, makampuni ya simu saba yalilipa jumla ya kodi
ya Shilingi Bilioni 101.7.
ya Shilingi Bilioni 101.7.
Julai, Augusti na Septemba 2017,
baada ya kuanza kutumika eRCS, Makampuni ya simu yale yale yameweza
kulipa Shilingi Bilioni 128.9. Kukiwa na ongezeko la Shilingi Bilioni
27.2 sawa na 21% ambazo ni majumuisho yaliyotokana na kodi ya Ongezeko
la thamani (VAT) na Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty).
Ukijumuisha makusanyo
yanayotokana na Kodi kutoka kampuni za simu saba kuanzia mwezi Aprili
2017 mapaka mwezi Septemba 2017 TRA imekusanya Jumla ya Shilingi Bilioni
230.7. kwa kipindi cha miezi sita tu, ambazo ni wastani wa shilingi
Bilioni 38.5 kwa mwezi.
Taarifa tulizopata kutoka chanzo
chetu ambao hawakutaka majina yao yatajwe wametueleza kwamba Serikali
inafuatilia kwa kina udanganyifu unaofanywa na kampuni za simu katika
Taarifa zao walizozipeleka TRA za input kwa ajili ya “return” ambazo
zinakosa uhalisia kwani zinajumuisha taarifa za miezi iliyopita kwa
lengo la kuongeza kiwango cha input tax.
Mfumo eRCS ulizinduliwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais
Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamad Shein walipozindua
Dirisha la kukusanya kodi Kielekroniki Elecrtronic Revenue Collection
System (eRCS) tarehe 1 Juni 2017, ukiwa na lengo la kusaidia Mamlaka
zote mbili za Mapato yaani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mamlaka ya
Mapato Zanzibar (ZRB) kuongeza mapato yanafanyika kupitia njia za
kielektroniki. Mpaka Mwezi Novemba 2017, ni kampuni saba za simu ndizo
zilizounganishwa katika mfumo wa eRCS, Kampuni hizo ni Vodacom, TTCL,
Airtel, tiGO, Halotel, Zantel na Smart.
No comments:
Post a Comment