Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Da es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………………………………………………………..
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amezitaka asasi za kiraia na madhehebu ya dini kuendelea kuongeza juhudi
katika kuchangia masuala yanayohusiana na ukimwi katika maeneo yao
ikiwemo kuhimiza maadaili na tabia njema katika jiamii.
Makamu wa Rais aliyasema haya wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais alisema kuwa kila mtu anapaswa kukumbuka kuwa jukumu kuu la
kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi linaanza na mtu
binafsi, jamii na hatimaye sote kama nchi.
“Ndugu
Wananchi Ukimwi umeendelea kuathiri nguvu kazi ya Taifa, wafanyakazi wa
taasisi za serikali na zisizo za serikali wanapata maambukizi kama wana
jamii wengine hii inapelekea kupungua kwa ufanisi makazini na kuathiri
uchumi kwa ujumla”
Makamu
wa Rais amezipongeza Taasisi zote ambazo zina mikakati ya kupambana na
ukimwi mahala pakazi kwa kuwakinga wafanyakazi wao na pia kuwahudumia
bila kuwabagua wala kuwanyanyapaa wale wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Makamu
wa Rais alisema Serikali ina nia thabiti ya kutafuta mikakati endelevu
ya kufikia TISINI TATU ifikapo mwaka 2020 na kumaliza kabisa ukimwi
ifikapo 3030.
Makamu
wa Rais alisisitiza kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha
miundo mbinu ya afya na kutoa mafunzo kwa wataalam wa afya ikiwa ni
pamoja na kuongeza watoa huduma kote nchini.
Makamu
wa Rais amesema Serikali imeanzisha mfuko wa ukimwi (AIDS TRUST FUND)
ukiwa na lengo la kuboresha rasilimali kwa ajili ya kuboresha huduma za
ukimwi yakiwemo matibabu, upimaji wa virusi vya ukimwi na kutokomeza
maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa motto pamoja, kuhudumia watoto
yatima na ujenzi wa vituo vya kutolea elimu ya ukimwi hivyo uwepo wa
mfuko huu utapunguza utegemezi na kuongeza kasi na ufanisi katika
mapambano dhidi ya ukimwi.
Makamu wa Rais alihimiza elimu ya ukimwi itolewe mashuleni ili vijana wawe na ufahamu wa kutosha .
Makamu
wa Rais alimaliza kwa kuwapongeza UNAIDS na wadau wote wanaoshiriki
katika mapambano dhidi ya ukimwi na kuwahakikishia serikali ipo pamoja
nao.
No comments:
Post a Comment