Eneo la ofisi ya Shirika la
Utangazaji la Taifa TBC linaloendelea na ujenzi lililopo Njiro mkoani
Arusha. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Bi.Susan P. Mlawi alitembelea eneo hilo kujionea maendeleo ya ujenzi
yaliyofikiwa leo Tarehe 28/12/2017
Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg.
Gerald G. Uisso (kushoto) akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi chumba kitakacho tumika
kama studio za TBC FM na TBC Taifa wakati alipo kagau maendeleo ya
ujenzi wa ofisi za kanda za shirika hilo zilizoko Njiro jijini Arusha
leo tarehe 28/12/2017. Bi Susan ametembelea eneo hilo kukagua hatua
zilizofikiwa katika ujenzi wa ofisi mpya za TBC kanda ya Arusha, ujenzi
huo unatarijiwa kukamilika mwezi januari 2018.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi (katikati) akimuelekeza
jambo Mkandarasi wa Kampuni ya Alkan CIT Ngd. Ali Mohamedi (Kulia)
wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya za Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC) zinazojengwa eneo la Njiro jijini Arusha leo
tarehe 28/12/2017. Kampuni ya Alkan CIT ndiyo inayojenga ofisi hiyo
ambapo ujenzi unatarijiwa kukamilia mwezi Januari 2018. Kushoto ni Mkuu
wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg. Gerald G. Uisso
Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg.
Gerald G. Uisso (kulia) akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi mtambo mpya wa kurushia
matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa wakati alipotembelea eneo ambalo
mtambo huo umefungwa mtaa wa Njiro jijini Arusha leo tarehe 28/12/2017.
Mtambo huo utaongeza usikivu wa TBC Fm na TBC Taifa kwa kanda ya
Arusha.
Msimamizi
wa Kituo cha kurushia matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa cha Namanga
mkoani Arusha Ndg. Joseph Nchinga (kushoto) akitoa maelekezo ya mtambo
mpya wakurushia matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa kwa Katibu Mkuu Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi (wa kwanza
kulia) wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo eneo la Namanga mkoani
Arusha leo tarehe 28/12/2017. Kituo hicho kimekamilika na kimeongeza
usikivu wa TBC Fm na TBC Taifa kwa umbali wa Kilomita 45 kwa pande zote
mbili za mpakani mwa Tanzania na Kenya.
PICHA NA
OCTAVIAN KIMARIO
WHUSM
No comments:
Post a Comment