Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Bw. Gerson Mdemu aliesimama akiwsilisha taarifa ya utekelezaji kwa
mwaka wa fedha 2016/2017 na kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha
2017/18 ya ofisi yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi katikati akiangalia nyaraka mbalimbali mezani wakati
alipokutana na kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
majukumu yake kwa Kamati hiyo mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Katba na Sheria Mhe. Mohamed Mchengerwa katikati akitabasamu baada ya
kumsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Kabudi wakati
alipokutana na watendaji wa Taasisi za Wizara waliokuwa wakiwasilisha
taarifa za utekelezaji wa taarifa hizo
………………..
Serikali imeokoa kiasi cha
Shilingi Bilioni 24,556,724,598 na Dola za Marekani 7,817,170.48
kupitia mashauri ya madai ambayo Serikali ilishinda yaliyoendeshwa
katika ...
mahakama mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Mdemu alipokuwa akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji ya ofisi yake kwa kipindi cha robo ya kwanza ya
mwaka wa fedha 2017/18 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
walipokutana mjini Dodoma.
Amesema wameiwezesha Serikali
Kushinda kesi kwenye mashauri 23 yaliyokuwa yanahusisha madai ya fedha
na kuongeza kuwa kama Serikali isingekuwa makini na kushindwa kesi
ingelipa kiasi cha shilingi 24,556,724,598 na na Dola za Marekani
7,817,170.48.
“Kama Serikali isingekuwa makini
na kushindwa kesi ingelipa kiasi cha shilingi 24,556,724,594 “Hivyo basi
kwa kushinda kesi hizo, Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi
24,315, 498,042.44 na Dola za Marekani 7,817,170.48 na hivyo kupoteza
kiasi cha shilingi 241,226,557.56, kwa kesi ilizoshindwa”, alifafanua.
Amesema ofisi yake imeendelea
kutekeleza kikamilifu jukumu lake la kutoa ushauri wa kisheria kwa
serikali na Taasisi zake na na kuwezesha utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo kama vile mradi ya bomba la mafuta kutoka Hoima
hadi Tanga ambayo italeta ajira na kuchangia mapato kwa Serikali.
Amesema Ofisi yake pia imeendesha
mashauri 169 ya kikatiba yakiwemo mashauri mapya 37 , mashauri hayo yote
yapo katika hatua mbalimbali ambapo Mashauri 25 yalihitimishwa na
kufanya kubaki mashauri 144 ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi .
No comments:
Post a Comment