Kamishna Msaidizi anayeshughulikia
Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Edward Ishengoma (kulia
waliokaa mbele) pamoja na wajumbe wengine akifuatilia maelezo yaliyokuwa
yanatolewa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James
(hayupo pichani) katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango, Dotto James (kulia) na Kamishna wa Maendeleo wa Umoja wa
Ulaya (EU), Neven Mimica (kushoto) wakisaini makubaliano ya msaada wa
Euro Milioni 50 kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya nishati nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango, Dotto James ( wa pili kushoto waliosimama mbele) na Kamishna
wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU), Neven Mimica ( wa tatu kushoto
waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe mara baada
ya utiaji saini wa makubaliano hayo.
……………..
Na Mwandishi wetu
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa msaada
wa kiasi cha Euro Milioni 50 ambazo ni sawa na takribani shilingi
bilioni 130 za kitanzania kwa ajili ya miradi ya usambazaji wa Umeme
Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Makubaliano ya msaada huo
yalisainiwa jijini Dar es Salaam tarehe 2 Novemba, 2017 kati ya Umoja
wa Ulaya (EU) ukiwakilishwa na...
Kamishna wa Maendeleo wa Umoja huo,
Neven Mimica na Serikaliya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na
Mipango ikiwakilishwa na Katibu Mkuu wake, Dotto James. Katika mkutano
huo, Wizara ya Nishati iliwakilishwa na Kamishna Msaidizi
anayeshughulikia Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma
Akizungumza kabla ya kusaini
makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto
James alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya awali ya kiasi
cha Euro Milioni 180 zilizotolewa kwa ajili ya kuboresha Sekta ya
Nishati na kufafanua kuwa fedha hizo zitatolewa katika Awamu
mbalimbali.
Alisema kuwa kati ya Euro Milioni
180, Euro Milioni 90 zitatumika kwa ajili ya mpango wa kusambaza Umeme
Vijijini kupitia REA na nyingine Euro Milioni 90 zitatumika kwa ajili
ya kuboresha Sekta ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) na REA.
Aliendelea kusema kuwa msaada huo
usio na masharti ni moja ya mikakati ya Umoja wa Ulaya (EU) kuunga
mkono juhudi za Serikaliya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John
Magufuli katika usambazaji wa Umeme Vijijini.
Katika hatua nyingine, James
aliushukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa msaada huo na kusisitiza kuwa
Serikaliitautumia msaada huo katika kuhakikisha kuwa vijiji vyote
Tanzania vinapata Umeme ifikapo mwaka 2020.
Awali akielezea mafanikio ya REA,
James alisema wakati REA inaanzishwa mwaka 2008 asilimia mbili tu ya
vijiji vyote vilikuwa vinapata Umeme lakini hadi kufikia Desemba, 2016
ni asilimia 49.3 wananchi waishio vijijini wanapata Umeme.
Aliendelea kufafanua kuwa mwaka 2008 asilimia 10 ya wananchi kitaifa walikuwa wanapata Umeme (overall electricity access level) lakini hadi kufikia Desemba, 2016 ni asilimia 67.5 wanapata Umeme wa uhakika.
“Mafanikio haya ni makubwa na
ninaamini kupitia msaada huu na ongezeko la kasi ya usambazaji wa Umeme
vijijini, ifikapo mwaka 2020 vijiji vyote nchini Tanzania vitakuwa
na Umeme wa uhakika na kupelekea kwenda kwenye uchumi wa Viwanda,”
alisema James.
Wakati huo huo
akizungumza kabla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Kamishna wa
Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU), Neven Mimica alisema kuwa Umoja huo
unatambua juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati
katika usambazaji wa Umeme vijijini hivyo wapo tayari kuisaidia
Serikaliili iweze kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa yenye
lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya kipato cha kati
ifikapo mwaka 2025.
Alisema kuwa Nishati ya Umeme ni
muhimu husan katika maeneo ya vijijini kwa kuwa inachangia uboreshaji
wa huduma za jamii kama Shule, Vituo vya Afya, Hospitali, Viwanda
vidogo vidogo na Kilimo.
Aliendelea kusema kuwa, kupatikana
kwa Umeme wa uhakika vijijini kutapelekea ongezeko la ajira kwa kuwa
wananchi wataweza kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya
kusindika mazao.
No comments:
Post a Comment