Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na baadhi ya watanzania waishio nchini Canada, kwenye hoteli
ya The Ritz-Carlton Toronto Oktoba 31, 2017
Watanzania waishio nchini
Canada,wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipo kutana
nao kwenye hoteli ya The Ritz-Carlton Toronto Oktoba 31, 2017.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
…………..
KUWENI WAZALENDO, WAZIRI MKUU AHIMIZA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waishio Canada wadumishe mshikamano wao na wawe na uzalendo kwa Taifa lao.
Ametoa wito huo jana (Jumanne, Oktoba 31, 2017) wakati akizungumza na Watanzania waishio Toronto, Canada.
Waziri Mkuu ambaye yuko
Canada kwa ziara ya ...
kikazi, alisema kila Mtanzania anapaswa ahubiri
utaifa wake. “Tembea huku ukiringia nchi yako, wakati wote ringia nchi
yako, unapotakiwa kuisemea nchi yako, isemee vizuri kama ambavyo wengine
wanasemea vizuri nchi zao licha ya matatizo waliyonayo.”
Aliwataka wakumbuke kuweka
akiba na wanapopata fursa watume fedha zao nyumbani ili zisaidie kuleta
maendeleo. “Ukipata kitu kidogo, rusha nyumbani; ukipata mtu anayeweza
kuleta tija, mlete nyumbani, nasi tutawapokea wewe na yeye,”
alisisitiza.
“Tunawasisitiza muitangaze
nchi yetu kwa mataifa mengine ili nao waone Tanzania ni mahali pa fursa,
na akitaka kuwekeza ajue kuwa anawekeza mahali ambapo ni salama,”
alisema.
Alisema Serikali inasisitiza
wananchi waishio nje ya nchi, wawe wazalendo na washirikiane kuhakikisha
wanazitumia vizuri fursa za kimaendeleo kwa manufaa ya nchi yao.
Awali, Balozi wa Tanzania
nchini Canada, Mhe. Jack Nzoka, alitumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania
waishio nchini humo wazingatie sheria za nchi hiyo.
“Wote sisi tunawatambua kama
mabalozi katika nafasi zenu hapa Canada. Tunawashauri muwe raia wema, na
muishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi hii na msisahau
mlipotoka, kwani hakuna mahali pazuri kama nyumbani,” alisisitiza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, NOVEMBA MOSI, 2017.
No comments:
Post a Comment