Timu ya Tottenham imefuzu kutinga
hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutandaza soka safi na
kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Real Madrid katika dimba la
Wembley.
Spurs, ikicheza ikiwa na nyota wake
mshambuliaji Harry Kane ambaye amerejea uwanjani baada ya kupona
maumivu ya paja, ilionyesha kiwango kizuri cha soka na alikuwa Dele
Alli aliyefunga goli la kwanza katika dakika ya 27.
Dele Alli tena akaifungia Tottenham
goli la pili katika kipindi cha pili kisha Christian Eriksen akafunga
goli la tatu akiunganisha kwa utulivu krosi ya Kane, kabla ya
Cristiano Ronaldo kufunga goli pekee la Real Madrid.
Mshambuliaji Dele Alli akifunga goli la kwanza la Tottenham
Cristiano Ronaldo akiwa ameshika kiuona baada ya jahazi ya Real Madrid kuzama
No comments:
Post a Comment