Timu ya Liverpool imekaribia kutinga
hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu
mwaka 2008-09 kwa kupambana mno na kuibuka na ushindi wa magoli 3-0
dhidi ya Maribor.
Mshambuliaji Mohamed Salah alikuwa
wa kwanza kutikisa nyavu kwa kufunga kifundi, huku baadaye James
Milner akishuhudia penati yake ikiokolewa na kipa Jasmin Handanovic
mwenye miaka 39.
Kiungo Emre Can aligongeana vyema na
Milner na kisha kuachia shuti la mpira wa kuzungusha uliomkuta Daniel
Sturridge aliyefunga goli la tatu.
Mohamed Salah akifunga goli la kwanza la Liverpool
Mshambuliaji Daniel
Sturridge akifunga goli la tatu la Liverpool
No comments:
Post a Comment