Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni
Bw.Hashim Mgandilwa akimkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula katika ofisi za Wilaya hiyo
kukagua mfumo mpya wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya
kielektroniki katika ziara yake ya kikazi leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akikagua orodha ya wadaiwa sugu
wa kodi ya pango la ardhi kwa Manispaa ya Kigamboni kulia ni Mkuu wa
Wilaya hiyo Bw. Hashim Mgandilwa na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa
hiyo Bw. Stephen Katemba katika ziara yake leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akikagua mafaili ya
umilikishaji ardhi katika Masjala ya Manispaa ya Kigamboni wakati wa
ziara yake katika Manispaa ya Kigamboni leo.
Maneja Masoko wa Kampuni ya
Ujenzi Makazi ya Hamidu City Park Bi. Judith Eminice (kulia) akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
Angelina Mabula (kushoto) kuhusu mradi wa ...
nyumba ulioko katika Manispaa
ya Kigamboni katika ziara yake kukagua mfumo mpya wa ukusanyaji kodi
pango la ardhi kwa njia ya kielektroniki leo Jijini Dar es Salaam.
Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Hashim Mgandilwa.
………………………………………………………………………………..
Na. Paschal Dotto-MAELEZO.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula ameitaka Halmashauri ya
Manispaa ya Kigamboni kusitisha utoaji hati kwa eneo la mradi wa kampuni
ya AVEC ambalo lina mgogoro wa umiliki ili kuepusha migogoro ya ardhi
iliyoko katika Manispaa hiyo.
Akizungumuza na watumishi wa
manispaa ya Kigamboni Mhe. Mabula alisema kuwa kwa maeneo ambayo bado
hayajapatiwa hati na vibali vya ujenzi wahakikishe yanatolewa hati
sahihi bila kuleta migogoro kwa wananchi.
“Migogoro ya ardhi mingi
husababishwa na utoaji hati bila kufanya uchunguzi wa umiliki wa maeneo.
Mkurugenzi na na watu wake wanaweza kukaa na kufanya upembuzi maalum
ili kutoa hati sahihi, bila kufanya hivyo msitoe hati maana hii ndiyo
husababisha kuwepo kwa migogoro ya ardhi kwenye Manispaa nyingi nchini”,
alisema Mhe. Mabula.
Aidha aliwataka watumishi wa
Manispaa hiyo kuwabana wamiliki wa viwanja mbalimbali ilikubaini kama
wana hati kamili na kulipa kodi ya ardhi ili kuiwezesha idara hiyo
kujiendesha katika shughuli zake lakini pia aliwaonya wasitoe hati hizo
kwa maeneo yenye utata.
“Kwa wale ambao wanajenga nyumba
za kawaida huwa ni miezi 36 na mashamba ni miezi 48 kwa hiyo kama
hajalipa kwa miezi yote hiyo anatakiwa kufikishwa kwenye Baraza Kuu,
sasa fanyeni ukaguzi wa maeneo yenu kwa sababu mji huu uko kwenye
mpango mji”, alisisitiza Mhe. Mabula.
Aliongeza kuwa katika ujenzi wa
mji huo, watumishi wanapaswa kuwajibika kuwaelimisha wananchi kujenga
kwa kufuata sheria za ujenzi ili kuondo usumbufu wa badae. Aidha, Naibu
Waziri aliwasisitiza watumishi hao kufanya ukaguzi ili kubaini watu
waliojenga vibali kwa sababu migogoro mingi katika Manispaa ya kigamboni
inasababishwa na watu kutokuwa na vibali.
“Mtu anaweza kuwa na kiwanja
halali na hati ya umiliki, lakini anapojenga amaepata kibali kutoka
Manispaa, kama hana kibali lazima mfuatilie, na lazima apigwe faini ili
alipe tozo zote za Serikali”, aliongeza Mhe. Mabula.
Akibainisha chanzo cha migogoro
Mhe. Mabula alisema kuwa katika Manispaa hiyo kumekuwa na
Wenyekiti wa vijiji kujiingiza katika ununuzi wa viwanja na utoaji hati
kitu ambacho kinaleta migogoro mingi kwa wananchi.
Aliwataka wenyeviti wa mitaa
kuacha kujihusisha kabisa na masuala ya umilikishaji wa ardahi ili
kuondoa migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Kigamboni.
No comments:
Post a Comment