Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima (TEWW) Dkt. Fidelice Mafumiko akisisitiza jambo kwa
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima kutoka Kouvola nchini
Finland Bi. Leena Kaivola wakati wa ziara yake katika Taaisisi hiyo leo
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima (TEWW) Dkt. Fidelice Mafumiko akieleza kwa Mtendaji Mkuu wa
Kituo cha Elimu ya Watu Wazima kutoka Kouvola nchini Finland Bi. Leena
Kaivola jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kutoa elimu kwa wale waliokosa
katika mfumo rasmi wakati wa ziara yake katika Taaisisi hiyo leo Jijini
Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Elimu
ya Watu Wazima kutoka Kouvola nchini Finland Bi Leena Kaivola akieleza
jinsi mpango wa elimu ya watu wazima unavyotekelezwa nchini humo wakati
wa ziara yake katika Taaisisi ya Elimu ya Watu Wazima leo Jijini Dar
es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uchapishaji
wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bw. Kasara Muganda akitoa maelezo
kuhusu maboresho yaliyofanywa na Taasisi hiyo kwa kununua mitambo mipya
ya uchapishaji wakati wa ziara ya Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Elimu ya
Watu Wazima kutoka Kouvola nchini Finland Bi Leena Kaivola na ujumbe
wake leo Jijini Dar es Salaam, ziara inayolenga kuimarisha uhusiano kati
ya Taasisi hizo mbili.
Mhadhiri wa Taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima Dkt. Sempeho Siafu akiwasilisha mada kuhusu mpango wa elimu
changamani baada ya msingi (IPPE) kwa ujumbe kutoka Kituo cha Elimu
ya Watu Wazima kutoka Kouvola nchini Finland wakati wa ziara yao katika
Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam mapema leo.
(Picha zote na TEWW)
…………………………………………………………………………
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
inatarajia Kushirikiana naTaasisi za Kimataifa katika Kukuza Kiwango cha
Elimu hapa nchini, hasa elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii.
Akizungumza wakati wa ziara ya
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima cha Kouvola cha nchini
Finland Bi.Leena Kaivola aliyeongozana na baadhi viongozi waandamizi wa
kituo hicho , MkurugenziwaTEWW Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa
ushirikiano kati ya Taasisi yake na Kituo hicho unalenga kukuza Elimu na
Utafiti ambao utakuwa na faida kwa pande zote mbili.
“Ushirikiano wetu unalenga kukuza
kiwango cha elimu kupitia utaratibu wa kubadilishana uzoefu na kituo
hiki cha Kouvola cha nchini Finland ambapo katika mazungmzo ya awali
tumekubaliana kushirikiana kwa kipindi cha miaka mitano”Alisisitiza Dkt.
Mafumiko.
Akifafanua Dkt. Mafumiko amesema
dhamira ya Taasisi yake ni kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu
wakiwemo wa ndani na nje ya nchi katika kutoa fursa za elimu kwa vijana
hasa wale waliopo nje ya shulena watu wazima kujipatia maarifa na ujuzi
stahiki hapa nchini kwa kuwa sekta hiyo ni moja ya vipaumbele vya
Serikali hasa katika kukuza maendeleo ya viwanda.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuuwa
Kituo cha Kouvola Bi. Leena Kaivola amesema kuwa Kituo chake kitajikita
katika kuimarisha ushirikiano katika kutekeleza malengo ya pamoja
yatakayoleta manufaa kwa pande zote mbili katika kukuza ushirikiano
utakaoleta tija katika sekta ya elimu.
Aliongeza kuwa Kituo chake
kinatekeleza majukumu yanayofanana na yale yaTaasisi ya Elimu ya Watu
wazima hali inayochochea kuwepo kwa ushirikianobaina yao.
No comments:
Post a Comment