Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia
Evarist Ndikilo akizungumza na wananachi na baaadhi ya viongozi mbali
mbali wa serikali mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda
hicho cha chaki cha Mkongoma kiichopo Wilayani Kisarawe
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha
chaki Geofrey Mkongoma akitoa risala fupi kwa mgeni rasmi mara baada
ya kiwanda hicho kuwekea jiwe la msingi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani .
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe
Happines Seneda akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za
uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha chaki.
Baadhi ya viongozi wa halmshauri
ya Wilaya ya Kisarawe wakiwa katika halfa hiyo ya uwekaji wa jiwe la
msingi katika kiwanda hicho cha chaki.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
…………….
NA VICTOR MASANGU, KIRASAWE
KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais
wa serikali ya awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na
uchumi wa viwanda,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo
amewataka wawekezaji wote kuhakikisha wanaachana kabisa na tabia ya
kukwepa kulipa kodi na badala yake watimize wajibu wao ipasavyo bila ya
kuvunja sheria na taratibu za nchi ili kuweza kuleta mabadiliko chanya
ya...
kimaendeleo kwa wananchi.
Injinia Ndikilo ametoa kauli hiyo
wakati wa halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha chaki
kinachoendelea kujengwa katika awamu ya kwanza katika kijiji cha Msanga
zalala kata ya Msimbu Wilayani Kisarawe na kuhudhuriwa na viongozi mbali
mbali wa , serikali, madhehebu ya dini pamoja na watendaji wa serikali
za vijiji na vitongoji.
Pia Mkuu huyo alibainisha kuwa
katika uwekezaji wa viwanda katika Mkoa wa Pwani baadhi ya maeneo bado
yanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa ni nishati ya umeme wa uhakika
pampja na kuwepo kwa mioundimbinu mibovu ya barabara hivyo ameagiza
mamlaka zote zinazohusika kulifanyia kazi suala hilo ili kuweza
kuwavutia wawekezaji wengine.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe
Happiness Seneda alitoa wito kwa wananchi wengine kutumia fursa zilizopo
katika kujifunza mambo mbali mbali ya ujasiriamali na kuanzisha
viwanda vidogo vidogo kwa lengo la kuweza kuunga juhudi za serikali ya
awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati pamoja na kuwapa nafasi zaidi
wawekezaji ambao ni wazawa ili waweze kutoa fursa za ajira kwa vijana.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa
kiwanda hicho cha chaki Geofrey Mkongoma akisoma taarifa yake ameiomba
serikali ya awamu ya tano kuweza kuwapa fursa ya kipekee wazawa wa
Tanzania katika suala zima la uwekezaji wa ujenzi wa viwanda
vidogovidogo huku akitaja akisema changamoto kubwa ni suaala la umeme wa
uhakika.
Alisema kuwa lengo lake kubwa ni
kuhakikisha anaunga mkono juhudi za serikali ya wamu ya tano katika kuwa
na uchumi wa viwanda hivyo ataendelea kushirikiana bega kwa began a
wadau wengine kwa lengo la kuweza kufanikisha malengo aliyojiwekea ya
kuweza kutoa fursa za ajira kwa wazawa pamoja na kuongeza uzalishaji wa
chaki.
“Hiki kiwanda kilianza tangu mwaka
2013 na kwa sasa kama mnavyoona mimi nimeshaajiri wafanyakazi wapatao
38. Ambao ninawalipa kutokana na kiwanda hiki cha chaki hivyo kitu
kikubwa ninachokiomba kwa serikali ni kutoa sapoti kubwa zaidi kwa
wawekezaji ambao ni wazawa ili waweze kuendelea kujenga viwanda vidogo
vidogo ili kuweza kukuza uchumi wa nchini,”alisema Mkurgenzi Mkongoma.
Nao baadhi ya wakinamama ambao
wanafanya kazi katika kiwanda hicho cha chaki akiwemo Tedy Mzingula na
Shoboa Msagasa wamesema kuwa kipato wanachokipata kinaweza
kuwabadilisha kwa kiasi kikubwa katika suala zima la kujikwmau kimaisha
kutokana na kuendesha familia zao ikiwemo kuwasomesha watoto walionao
pamoja na kuwahudumia mahitaji madogo madogo.
“Sisi kwa kwli kama wafanyakazi wa
kiwanda hiki tunapenda kumshukuru Mkurugenzi wetu kwa kuweza kupenda
katika hali na mali, na kutokana na kufanya kazi hii fedha ambayo
tunaipata inatusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendesha familia zetu,
kwani wengne tuna watoto ambao tunawasomesha na maisha yanaendelea
lakini kikubwa ni serikali kumsaidia kuweza kupata umeme,”walisema.
KIWANDA hicho cha chaki ambacho
kinajulikana kwa jina la Mkongoma Chalk Factor kilianzishwa mnamo mwaka
2013 ambapo kwa sasa kina jumla ya wafanyakazi zaidi ya 38 wakiwemo
vijana pamoja na wakinamama kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo ya
Kisarawe.
No comments:
Post a Comment