Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Jensen Msechu (kushoto)
akisimika moja ya miamvuli iliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya
Zantel kwa Chuo cha Ustawi wa Jamii hivi karibuni jijini Dar es
salaam.Jumla ya Miamvuli 60 ilitolewa kwa chuo hicho kwa lengo la
kuwakinga jua wanafunzi wakati wa kujisomea wawapo chuoni hapo. Katikati
ni Afisa Rasilimali watu Mwandamizi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii,
Remidius Leonard na kulia ni Rais wa Wanafunzi, John Filimon.
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kilichopo eneo la Bamaga
jijini Dar es salaam wakijisomea kwenye moja ya kizimba kilichosimikwa
moja ya miamvuli iliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel hivi
karibuni jijini Dar es salaam. Jumla ya miamvuli 60 ilitolewa kwa ajili
ya kuwakinga jua Wanafunzi wa chuo hicho wakati wa kujisomea wawapo
chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment