Manchester United imeibuka na
ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Benfica katika mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford.
Manchester United ilipata goli lake
la kwanza kupitia kwa Mile Svilar ambaye alijifunga na kisha kuongeza
goli la pili kupitia penati iliyofungwa na Daley Blind.
Katika mchezo huo Manchester United
pia ilikosa penati moja iliyopigwa na Anthony Martial iliyopatikana
baada ya beki kuunawa mpira.
Romelu Lukaku akijiandaa kupiga penati lakini kocha Jose Mourinho akatoa maagizo apige Daley Blind
Daley Blind akipiga penati na kufunga goli la pili la Manchester United
No comments:
Post a Comment