Chelsea imekuwa timu ya kwanza ya
Uingereza kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu huu
baada ya kufungwa magoli 3-0 na wenyeji Roma.
Roma walipata goli la kwanza kupitia
kwa Stephan El Shaarawy, kwa shuti la umbali wa yadi 25, kisha
baadaye Alvaro Morata akakosa nafasi ya kusawazisha.
El Shaarawy tena akafunga goli la
pili baada ya beki Antonio Rudiger kushindwa kuudhibiti mpira
uliopigwa na Radja Nainggolan, kisha Diego Perotti akafunga goli la
tatu.
Stephan El Shaarawy akifunga goli la kwanza la Roma
Diego Perotti akiwa ameachia shuti lililozaa goli la tatu
No comments:
Post a Comment