Beki wa kushoto Layvin Kurzawa
amekuwa beki wa kwanza kufunga magoli matatu yaani hat-trick wakati
Paris St-Germain ikiichakaza Anderlecht kwa magoli 5-0 katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Beki Kurzawa alikuwa amefunga magoli
17 tu kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa jana usiku alifanikiwa
kupachika magoli hayo matatu katika kipindi cha pili.
Mbrazil Neymar na Marco Verratti nao
pia walifunga magoli mawili mazuri na kuifanya PSG na kufuzu hatua ya
mtoano.
Marco Verratti akiwa ameachia shuti lililozaa goli
Beki Layvin Kurzawa akiwa amefunga goli lake la pili kati ya matatu
No comments:
Post a Comment