Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya
Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdallah akiwasilisha mada kwa wajumbe wa
kamati ya kutokomea Kipindupindu Zanzibar.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kutokomeza Kipindupindu Zanzibar wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwakilishwa katika mkutano huo.
Mhadhi wa Chuo Kikuu cha Taifa
Zanzibar SUZA Dkt. Yahya Hamad Shehe akiwaeleza wajumbe wa mkutano huo
kuhusu mradi wa kupiga ramani mpya ya Zanzibar kwa kutumia ndege maalumu
kukusanya taarifa muhimu.
Afisa Habari wa Shirika la UNICEF
kutoka Nairobi Maureen Khambira akitoa mchango wake katika mkutano wa
kupambana na kipindupindu Zanzibar uliofanyika ukumbi wa uzazi salama
Kidongochekundu.
Picha na Makame Mshenga.
………………..
Zanzibar itaendeleza juhudi za
kupambana na maradhi ya kipindupindu ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2027
maradhi hayo yanatokomezwa lakini nguvu za pamoja za Taasisi za ndani
na nje ya nchi likiwemo Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) zinahitajika
kufanikisha juhudi hizo.
Mkurugenzi Tiba na Elimu ya Afya
Dkt. Fadhil Mohd Abdalla alieleza hayo alipokuwa akizungumza katika
mkutano wa siku mbili uliozishirikisha taasisi za ...
Serikali na taasisi za
kiraia katika ukumbi wa uzazi salama Kidongochekundu.
Alisema Wizara ya Afya imeamua
kuunganisha sekta mbali mbali za Serikali, za kirai na washirika wa
maendeleo wakielewa kuwa kipindupindu hakiwezi kumalizika kwa nguvu za
Wizara peke yake.
Aliwataka wajumbe wa mkutano huo
kila mmoja kwa nafasi ya taasisi anayotoka kuandaa mpango mkakati
utakaosaidia kumaliza kabisa kipindupindu Zanzibar ifikapo mwaka 2027.
Alisema Wizara ya Afya inafahamu
uzito uliopo wa kufanikisha mpango huo ikiwemo miundombinu isiyoridhisha
ya kupatikana maji safi na salama, ujenzi holela katika baadhi ya mitaa
na jamii kutokuwa tayari kubadili tabia.
“Jamii kukubali kubadili tabia ili
kwenda sambamba na mpango huu nina imani malengo ya kumaliza cholera
yanaweza kufikiwa,” alithibitisha Mkurugenzi Tiba.
Dkt. Fadhil alikumbusha kwamba
Wizara bado inaendeleza masharti ya afya katika kufanya biashara za
vyakula na biashara za vinywaji ambayo ni moja ya vyanzo vikubwa vya
kuibuka kipindupindu.
Akizungumza katika mkutano huo
Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andermichael aliwakumbusha
wananchi kufuata masharti ya afya ikiwemo kutumia vyoo, maji
yaliyochemshwa ama yaliyotibiwa na kunawa mikono kabla na baada ya kula.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar (SUZA) Dkt. Yahya Hamad
Shehe alisema katika kuchangia kumaliza cholera, Chuo kinaendeleza mradi
wa kupiga ramani mpya ya visiwa vya Zanzibar kwa kutumia ndege maalumu
ili kujua sehemu zinazopata maradhi hayo mara nyingi na sababu zake.
Alisema ramani hiyo mpya
itakusanya taarifa zote muhimu za Wilaya, shehia na mitaa ili kupata
urahisi wa kushughulikia tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment