Pages

Thursday, November 2, 2017

NHIF YATAKIWA KUONGEZA IDADI YA WANACHAMA NCHINI. NA WAMJW-DAR ES SALAAM


1
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati akifuatilia maelekezo yanayotolewa na mfanyakazi wa NHIF  alipotembelea  Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Bw. Bernard Konga.
2
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kulia akiangalia moja ya mafaili ya kuhifadhia kumbukumbu za madai katika ofisi za NHIF alipotembelea  Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam, wa kwabnza kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Bw. Bernard Konga.
3
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kulia akipata maelekezo kuhusu kitengo cha huduma kwa wateja kutoka kwa Mkuu wa kitengo hicho Bi. Anjela Mziray wa kwanza kushoto juu ya huduma zitolewazo na kitengo hiko alipotembelea NHIF leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Bw. Bernard Konga.
4
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile aliyesimama akiongea na watumishi wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF hawapo pichani alipotembelea  Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Bw. Bernard Konga.
5
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini NHIF Bw. Bernard Konga aliyesimama akiongea na watumishi wa taasisi hiyo hawapo pichani anayefuata aliyekaa ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile .
6
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini NHIF Bw. Bernard Konga aliyesimama akimuonesha Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baadhi ya tuzo walizopata katika kutoa huduma bora leo jijini Dar es salaam.
7
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia kitabu kinachohusu huduma za NHIF alichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo  Bw. Bernard Konga katikati wakati ziara yake katika taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.
8
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini NHIF wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.
Picha na WAMJW
……………..
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
MFUKO wa Bima ya Afya NHIF imetakiwa kufanya bidii katika kuongeza wanachama wa mfuko huo ili kufanya huduma za matibabu kupatikana kwa urahisi na gharama nafuu kwa watanzania wote.
Akizungumza na uongozi pamoja na watumishi wa...
Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa kuna umuhimu wa NHIF kuongeza wanachama wa mfuko huo.
“NHIF waweke uwezekano wa kuanzisha bima ya afya kwa wajawazito kwa bei nafuu hadi kufikia Julai 2018 na pia huduma hii kuwa ya lazima kwa wananchi wote ili kuwasaidia  kuepuka gharama kubwa za matibabu”  alisema Dkt. Ndugulile
 Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa NHIF wanatakiwa kutengeneza mpango wa kuondoa adha kwa wagonjwa wenye kadi za bima za mfuko huo kunyanyapaliwa kwa kuwa hawana hela ya malipo papo hapo ili waweze kupata matibabu stahiki kwa wakati.
Kwa mujibu wa Dkt. Ndugulile amesema kuwa sio lazima wananchama wa mfuko huo wawe watumishi wa umma bali waangalie hata sekta binafsi ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa maendeleo ya sekta ya afya nchini.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuweza kufanikiwa kuondoa rufani za nje kunatakiwa kutengenezwa sheria ya kupandikiza viungo kama vile figo,moyo,vifaa vya usikivu  na vinginevyo ili kuleta mabadiliko katika sekta ya afya hivi sasa na miaka ijayo kwani wataalamu watazalishwa hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini NHIF Bw. Bernard Konga amesema kuwa wamejidhatiti kuongeza wananchama wa mfuko huo kwa sekta mbalimbali na katika kutekeleza hilo wameanza mazungumzo na vyama vya ushirika ili kujua namna ya kuwasaidia wanachama wake.
“Tulishajipanga katika kutekeleza agizo hilo kwani mpaka hivi sasa tumeanza kuongea na vyama vya ushirika ikiwamo vyama vya wazalishaji korosho ili kuona uwezekano wa kuwasaidia katika kupata huduma hiyo” alisema Bw. Konga.
Aidha Bw. Konga amesema kuwa wapo bega kwa began a Seikali  katika kutekeleza sera ya afya kwa kutoa huduma ya kulipia matibabu kwa kila mtanzania aliyejiunga na mfuko huo  ili kuweza kufikia malengo ya sera hiyo mpaka kufikia 2020.
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo alitembelea makao ya  Mfuko wa Bima  ya Afya NHIF na kuongea na Uongozi,watumishi pamoja na kutembelea sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu za wadai,kituo cha huduma kwa teja na sehemu ya Tehama.

No comments:

Post a Comment