Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii Mhe. Peter Selukamba (kushoto)
akifungua kikao cha wizara na kamati hiyo kujadili maendeleo ya Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo
Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bi. Pamela Palangio
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza wakati wa kikao
cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii
kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na
maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Bibi. Joyce Fissoo akiwasilisha taarifa ya Bodi ya Filamu wakati wa
kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na
Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na
maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.
Mhe. Grace Tendega (kulia)
akichangia mada wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.
Kushoto ni Mhe. Sikudhani Chikambo
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akiwasilisha taarifa ya Basata
wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na
Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi (kulia) pamoja na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus
Willium (kushoto) wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha wizara na
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili
maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya
Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
………………
Na Genofeva Matemu, WHUSM, Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka Bodi ya Filamu pamoja
na Baraza la Sanaa la Taifa kuendelea kusimamia kazi za sanaa na filamu
ili ziweze kukidhi soko la...
ndani na la kimataifa.
Waziri Mwakyembe amesema hayo leo
Mjini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu.
“Bodi ya Filamu na BASATA wamekua
wakifanya kazi nzuri ya kukinua vipaji katika tasnia ya filamu na muziki
nchini. Ni wajibu wenu sasa kuendelea kusimamia tasnia hizo ili ziweze
kukidhi matakwa ya nchi yetu pamoja na kuitangaza nchi kimataifa”
amesema Mhe. Mwakyembe
Kwa upande wake Mhe. Grace Tendega
amezitaka taasisi hizo kuweka mikakati thabiti ya kusimamia tasnia ya
filamu na muziki hatua itakayowasaidia wanatasnia hizo kuboresha maudhui
ya maadili katika kazi filamu na muziki
Naye Mhe. Kasuku Bilago ameitaka
Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya filamu nchini kwani sekta hiyo
inayofasi kuhimu katika kuinua uchumi wa nchi kwa kasi zaidi kama ilivyo
katika nchi za wenzetu
Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Selukamba amewataka
wajumbe wa kamati hiyo kuwa na ushirikiano na Serikali katika kubadili
mtazamo wa kukuza sekta ya filamu na muziki nchini
No comments:
Post a Comment