Timu ya Wataalam kutoka Tanzania
wakifuatilia kikao cha Kamati ya Nishati cha Baraza la Kisekta la
Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katikati mbele ni Kamishna
Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia masuala ya Nishati na Kiongozi wa
Timu ya Wataalam wa Tanzania James Andilile, wa kwanza kushoto ni
Mtaalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Eliabi Chodota na kulia ni Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati Mhandisi
Styden Rwebangila.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki upande wa Sekta za Kijamii na Uzalishaji, Christophe
Bazivamo (kulia) na Mwenyekiti wa mkutano kutoka nchini Uganda Kaimu
Kamishna kutoka Idara ya Petroli, Utafiti na Uzalishaji nchini humo,
Honey Malinga, (kushoto) wakifuatilia kikao hicho.
Wataalam mbalimbali kutoka Tanzania wakifutilia kikao hicho.
Wataalam mbalimbali kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda na wakifuatilia kikao hicho.
Wataalam mbalimbali kutoka Tanzania akifuatilia kikao hicho.
……………
Na Asteria Muhozya,Arusha
Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta
la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaendelea katika siku
yake ya Tatu , Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.
Kamati ya Nishati ya Baraza hilo
imekutana ...
Oktoba, 2017, ambapo Kamati hiyo imepitia na
kujadili masuala yote yaliyoibuliwa katika Vikao vya Timu ya Wataalam wa
nchi Wanachama.
Mkutano huo ulianza na Timu za
Watalaam wa Nishati kutoka nchi Wananchama tarehe 30 Oktoba,2017 ambapo
masuala kadhaa kuhusu Sekta ya Nishati ikiwemo Gesi, Mafuta, Umeme,
Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati yalijadiliwa.
Akizungumza katika kikao cha
Kamati ya Nishati cha Baraza hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki upande wa Sekta za Kijamii na Uzalishaji, Christophe
Bazivamo amesisitiza umuhimu wa nishati kwa jumuiya hiyo na kuongeza
kuwa, nchi wanachama wanapaswa kuzingatia kuwa nishati hiyo ndiyo
kichocheo kikuu cha ukuaji uchumi kwa jumuiya hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
mkutano huo ambayo ni nchi ya Uganda, akizungumza katika mkutano huo,
Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Petroli, Utafiti na Uzalishaji nchini
humo, Honey Malinga, amewataka washiriki kutoka na ripoti nzuri ambayo
itawezesha utekelezaji wa programu mbalimbali katika Sekta ya Nishati
zilizopangwa kutekelezwa na jumuiya hiyo.
Aidha, amewataka kuyachukulia kwa
uzito masuala yote yanayojadiliwa katika kikao hicho kwa kuwa yanalenga
kuwezesha maendeleo na ukuaji uchumi kwa jumuiya hiyo.
Mapendekezo yanayojadiliwa
katika kikao cha Kamati ya Nishati cha Baraza hilo, yanatarajiwa
kuwasilishwa katika Kikao cha Makatibu Wakuu wa nchi wanachama tarehe 2
Novemba, 2017, kabla ya kuwasilishwa katika kikao cha Mawaziri wa
Nishati ifikapo tarehe 3 Novemba,2017.
Nchi wanachama zilizowakilishwa
katika Mkutano huo ni Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya na Burundi ambapo
Mwenyekiti wa Mkutano ni nchi ya Uganda na Katibu wa mkutano huo ni
Rwanda.
Tanzania katika mkutano huo,
inawakilishwa na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Mazingira na Nishati ya Zanzibar,
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa
Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta , Zanzibar (ZURA).
No comments:
Post a Comment