Pages

Tuesday, October 31, 2017

TIMU YA REAL MADRID YAIBISHWA NA GIRONA LA LIGA

Mabingwa watetezi Real Madrid wamepata kipigo cha aibu katika ligi ya La Liga kutoka kwa Girona na sasa wapo pointi nane nyuma ya vinara wa ligi hiyo Barcelona.

Goli la kisigino lililofungwa na kiungo Portu liliwapa ushindi Girona katika kipindi cha pili, baada ya kupita dakika nne tangu Cristhian Stuani kusawazisha.

Beki wa Manchester City anayecheza kwa mkopo Pablo Maffeo na Portu mashuti yao yaligonga mwamba. Goli la Real Madrid lilifungwa na Isco.
                                        Isco akifunga goli pekee la Real Madrid katika mchezo huo 
  Sergio Ramos akishika paji lake la uso kwa aibu huku akifunga macho baada ya kipigo

No comments:

Post a Comment