Burnley imechagiza sherehe za kocha
wake kutimiza miaka mitano akiinoa klabu hiyo kwa kupata ushindi wa
goli 1-0 dhidi ya Newcastle katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Zawadi ya ushindi huo kwa kocha Sean
Dyche, ilitokana na goli pekee katika mchezo huo lililofungwa na Jeff
Hendrick.
Mapema Newcastle walikaribia goli la
wapinzani wao pale Ayoze Perez alipopiga shuti la kuzungusha na
kupanguliwa na kipa Nick Pope.
Jeff
Hendrick akiifungia Burnley goli pekee katika mchezo huo
Kipa wa Burnley Nick Pope akiwa amedaka mpira huku Christian Aku wa Newcastle akimruka
No comments:
Post a Comment