Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini
Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini
Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (kulia) akimsikiliza Mheshimiwa Abdullah Makame (katikati) ambae
ni kiongozi wa msafara wa Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini
Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la
Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania baada ya kumalizika kwa
kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. ujumbe huo
uliongozwa na Mheshimiwa Abdullah Makame (wa tatu kulia) ambae ni
kiongozi wa msafara huo.
PICHA NA OFISI YA BUNGE
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna
Mstaafu Zelote Stephen ameishauri benki ya NMB kufungua tawi katika
bonde la Ziwa Rukwa ili kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi ambao
shughuli zao kubwa za kiuchumi ni kilimo cha mahindi, mpunga pamoja na
uvuvi.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo
kutaepusha matukio ya uvamizi na mauaji yanayofanywa na baadhi ya watu
wanaowavizia wakulima na wafanyabiashara wanaoweka fedha majumbani mara
tu baada ya mauzo ya mazao yao.
“Mimi nashauri Benki ya NMB muwe
na Tawi huku, si lazima kuwa na jengo, hata ile Mobile Banking ambayo
mwananchi anaweza kupata huduma zote za kuweka na kutoa fedha katika
gari hiyo, ili fedha zao hawa ziwe katika mikono salama,” Mh. Zelote
Alisema.
Ametoa ushauri huo katika ufunguzi
wa siku ya huduma kwa wateja iliyofanywa na benki ya NMB kanda ya
nyanda za juu katika Kijiji cha Mfinga, kata ya Mfinga, Wilaya ya
Sumbawanga, kabla ya kukabidhi vifaa vya shule pamoja na hospitali
vyenye thamani ya Shilingi milioni 20.
Sambamba na hilo Mh.Zelote
amewahamasisha wakulima pamoja na wafanyabiashara wa Kata ya Mfinga
kufungua akaunti benki na pia kujiunga katika vikundi ili kuwa na
urahisi wa kupata mikopo na kuweza kuwainua kiuchumi.
“Mbali na kuhifadhi fedha pia
benki inatoa mikopo kwaajili ya kujiendeleza na hatimae kuwainua
wakulima waweze kuongeza thamani ya mazao yao na kupata soko pana hasa
katika awamu hii inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli
inayohamasisha uchumi wa viwanda kwa taifa,” Alisema.
Aidha aliwataka viongozi wa Kijiji
na wanufaika wa vifaa hivyo kuvitumia vifaa hivyo kwa malengo
yaliyokusudiwa, ikiwemo kuwahudumia wananchi bila ya bugudha na kuonya
kuwa wananchi wasiogope kuwashitaki watumishi wanaowahudumia kwa viburi.
Awali akisoma taarifa fupi ya
Benki ya NMB Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja makao makuu ya benki hiyo
Richard Makungwa alisema kuwa Benki ya NMB hutenga asilimia moja ya
mapato kwa mwaka ili kuirudishia jamii na kuweza kuisaidia katika mambo
mbalimbali ikiwemo elimu na afya.
“Kwa kuunga mkono juhudi za Rais
wetu tumeamua kama Benki kutoa kompyuta 7, vitanda 8 vya kulalia,
vitanda 4 vya kujifungulia, magodoro 8 pamoja na mabati 204 vyote vikiwa
na thamani ya shilingi milioni 20 vilivyotolewa na benki hiyo kama
marejesho ya faida kwa wateja watu,” Alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kijiji hicho Godfrey Kalungwizi aliahidi kuvisimamia vifaa hivyo na
kuendelea kuwahamasisha wananchi kuchangia katika shughuli za
kimaendeleo.
NMB2 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akikabidhi
Kompyuta kwa Afisa Elimu Manispa ya Sumbawanga Silvestor Mwenekitete
katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja katika Kijiji cha Mfinga,
Wilayani Sumbawanga.
NMB3 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akikabidhi
vitanda kwa mganga mfawidhi zahanati ya Mfinga Ephraim Matekele (shati
ya draft) katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja katika Kijiji cha
Mfinga, Wilayani Sumbawanga.
NMB4 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akikabidhi
vitanda kwa mganga mfawidhi zahanati ya Mfinga Ephraim Matekele (shati
ya draft) katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja katika Kijiji cha
Mfinga, Wilayani Sumbawanga.
NMB5 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akiendeleza
ujenzi kwa kuweka tofali katika jengo la shule ya msingi Mfinga
waliopewa mabati 204 na Benki ya NMB.
NMB6 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) katika picha ya
pamoja na viongozi wa NMB pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mfinga,
Wilayani Sumbawanga.
No comments:
Post a Comment