Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Paul Makonda akiongea machache wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es salaam leo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala
za Mitaa Tanzania (ALAT) Bw. Gulma Hafeez Muccadam akisoma risala yao
mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa
Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jaffo
mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa
Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Waziri Mkuu Mhe Kassim majaliwa
akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa
Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ya
kumbukumbu na wadau wa maendeleo na wafadhili wakuu wa Mkutano Mkuu wa
33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) baada ya kuufungua
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji
wa benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa
33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa ALAT
Bw. Stephen Mhapa baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mstahiki Meya wa Dar es
salaam Mhe. Isaya Mwita Baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya
ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia ngoma ya Kigogo wakati
akiwasili kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa
Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea banda la benki ya NMB na
mabanda mengine kabla ya kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
PICHA NA IKULU
Na. Paschal Dotto- MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watendaji wa Serikali za
Mitaa kusimamia wananchi wao kulipa kodi ili kuimarisha huduma za jamii
kwa watanzania kwani kodi itaongeza mapato na kuboresha huduma za jamii.
Akizungumza leo jijini Dar es
Salaam katika...
mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa, (ALAT)
Rais Magufuli amesema kuwa ili nchi iweze kuendelea kiuchumi lazima
wananchi wake walipe kodi kwani hicho ni miongoni mwa chanzo muhimu cha
mapato ya Serikali kinachoiwezesha kuwapatia wananchi huduma nzuri na
bora.
“Tulianza kuimarisha ukusanyaji wa
mapato na kudhibiti ubadhirifu wa fedha za umma, tulibana mianya ya
ukwepaji kodi na kuongeza ukusanyaji mapato kutoka bilioni 800 kwa mwezi
hadi trilioni 1.3 kwa mwezi” Rais Magufuli alieleza.
Alifafanua kuwa kutokana na
ongezeko hilo Serikali sasa inaweza kulipa mishahara kwa wakati huku
ikilipa madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ilikuwa inaidai
Serikali shilingi trilioni 1.3 ambapo hadi sasa imeshalipwa shilingi
trilioni 1.2.
Rais Magufuli alieleza kuwa katika
utendaji kazi wa ALAT mkutano huo ni muhimu kwa serikali anayoiongoza
kwani Jumuiya hiyo ni mhimili muhimu wa kuwaunganisha wananchi na
serikali yao hivyo mkutano huo kwa nchi yetu una umuhimu wa kipekee.
“Kwangu mimi mkutano huu ni muhimu
sana kwa sababu ALAT ni chombo kinachounganisha mamlaka na wadau
wanaohusika na masuala ya Serikali”, alisisitiza Rais Magufuli.
Akibainisha miradi iliyotekelezwa
mpaka sasa kutokana na mapato ya wananchi, Rais Magufuli alisema kuwa
huduma ya elimu imeboreka zaidi baada ya serikali kuanza utaratibu wa
kutoa shilingi bilioni 18 kwa mwezi katika mwaka wa fedha 2015-2016.
Kufuatia hatua hiyo alisema idadi
ya watoto waliojiandikisha kuingia darasa la kwanza ilifikia asilimia 95
huku kidato cha kwanza wanafunzi wakiongezeka kwa asilimia 30 ambapo
alisisitiza kuwa uwezo huo umetokana na kuimarika kwa ukusanyaji wa
mapato.
Rais Magufuli aliwaambia wajumbe
wa mkutano huo kuwa katika kutekeleza mpango wa Serikali ya Awamu ya
Tano wa kuimarisha miundombinu, serikali imeshatia saini mkataba wa
ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam mpaka Makutupora Dodoma,
ambapo kwa awamu ya kwanza itaanzia Dar es Salaam mpaka Morogoro. Mradi
huu mkubwa utagharimu kiasi cha fedha za kitanzania shilingi trilioni
7.062 ambazo kwa asilimia 100 ni fedha za serikali kutoka kwa wananchi
walipa kodi.
Alitaja miradi mingine kuwa ni
upanuzi wa bandari mbalimbali za mizigo zikiwemo bandari za Mtwara
bilioni 130, Dar es Salaam bilioni 926.2, Tanga bilioni 16 pamoja na
ukarabati wa meli za mizigo katika Ziwa Nyasa na Ziwa Viktoria ambapo
pesa zote hizo ni za serikali kwa asilimia 100.
Akijibu risala ya ALAT, Rais
Magufuli ameipongeza Jumuiya hiyo na kuwataka wapambane na wasiogope
katika kutenda na kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.
Naye Mwenyekiti wa ALAT,
Gulamhafeez Mukadam ameiomba Serikali kutenga na kupeleka kwa wakati
ruzuku katika Halmashauri zao ili waongeze ufanisi katika kazi ya
kuwatumikia wananchi na kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kauli mbiu ya mkutano huo wa 33 ni
“Ardhi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ni chachu ya maendeleo,
Halmashauri zitenge ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vidogo na
vikubwa” ambapo Mukadam alisema kuwa kauli mbiu hiyo inakwenda sambamba
na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda.
ALAT ilianzishwa 1984 kwa lengo la
kuwakutanisha pamoja watendaji wa Serikali za Mitaa ili waweze
kubadilishana uzoiefu masuala ya utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment