MAKAMU wa Rais Mhe. SAMIA SULUHU
HASSAN, amezinduzi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka
2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10
kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, tukio litakalofanyika Makao
Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
Makamu wa Rais ametoa wito kwa watoa
huduma ndogo za fedha kupunguza riba za mikopo na tozo mbalimbali ili
kufanikisha lengo la Sera hiyo ambalo ni kuimarisha huduma jumuishi
za fedha kwa kujenga mazingira wezeshi yatakayoleta ufanisi wa utoaji
wa huduma ndogo za fedha nchini kwa wananchi wenye kipato cha chini.
“Ninawaomba pia muongeze ubunifu
katika kutoa huduma zinazohitajika na wananchi wa kipato cha chini
pamoja na kupeleka huduma hizo katika maeneo yaliyo karibu na makazi
yao au biashara zao” aliongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan
Alizitaka taasisi za huduma za
fedha kuwaelimisha wananchi kabla ya kutoa huduma hizo ili kupunguza
athari wanazozipata wananchi.
“Ni matarajio yangu kuwa, Wizara
ya Fedha na Mipango itashirikiana na wadau katika kutekeleza Sera hii
na kuhakikisha malengo ya Sera ambayo ni kukuza uchumi na kupunguza
umaskini yanafikiwa” alisisitiza
No comments:
Post a Comment