Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba,akibadilishana nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la
Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya(kulia)
zenye makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi
wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa
wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere,jijini Dar es
Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu
ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, akibadilishana
nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)
nchini Tanzania, Chansa Kapaya (kulia) zenye makubaliano juu ya Mpango
wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani
Kigoma.Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Nchemba.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Wajumbe kutoka Serikali ya
Burundi wakiongozwa na Balozi wa Burundi nchini Tanzania,Gervais Abayeho
wakiwa katika Mkutano wamakubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha
Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo
yamefanyika mwishoni mwa wiki,Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius
Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Wajumbe kutoka Mashirika
mbalimbali ya kimataifa wakiwa katika Mkutano wa makubaliano juu ya
Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani
Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
…………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Wakimbizi wa Burundi waliokimbia
machafuko nchini kwao wataanza kurejea nchini kwao ifikapo Septemba 7
hadi Desemba 31, mwaka huu mara baada ya pande tatu ikiwemo Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia
Wakimbizi Duniani (UNHCR), kutiliana saini Mpango wa Kuwarejesha
wakimbizi baada ya mkutano uliochukua takribani siku tatu katika kuandaa
mpango huo.
Wakitiliana saini makubaliano
hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka
nchini Burundi, Pascal Barandagiye na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia
Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya, mwishoni mwa
wiki wote walikubaliana kutekeleza vipengele vilivyopo katika
makubaliano hayo yakiwa na lengo la kuwarudisha wakimbizi walioomba
kurejea nchini Burundi, baada ya hali ya Amani na utulivu kurejea.
Akizungumza baada ya kutiliana
saini makubaliano hayo Waziri Mwigulu, alisema umefika wakati wa
wakimbizi wa Burundi kurudi nchini kwao kuungana na familia zao na ndugu
waliobaki ili kusaidia kujenga uchumi wa nchi yao baada ya kuwa katika
machafuko yaliyosababisha kukimbia nchi yao kwa muda mrefu.
“Mimi kama mwanauchumi ninaona
madai yao ya kurudi nchini Burundi kujishughulisha na shughuli za kilimo
ni maamuzi mazuri huku pia wakisisitiza kurejea kwa Amani na Utulivu
nchini kwao kuwa ni sababu ya msingi ya kufikia kuomba kurejea, sisi
kama Serikali tutahakikisha zoezi hilo la urejeaji nchini kwao linaenda
salama tukishirikiana na Serikali ya Burundi kupitia Wizara ya Mambo ya
Ndani ya nchini Burundi,” alisema Mwigulu.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani na
Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, amesema
anaishukuru Serikali ya Tanzania na Watanzania wanaoishi kwenye maeneo
yaliyotumika kuwahifadhi wakimbizi kwa ukarimu wao walioonyesha muda
wote kwa raia kutoka nchini Burundi huku akisisitiza kurejea kwa hali ya
Amani na utulivu ambao hapo mwanzoni ilitoweka.
“Nawaomba wananchi wetu warejee
nchini ili tuweze kuijenga Burundi yetu ambayo hivi sasa kuna Amani na
utulivu, pia naishukuru Serikali ya Tanzania na Watanzania ambao wamekua
wakiwaonyesha ukarimu wakimbizi kutoka Burundi na kuwapa hifadhi
nchini hapa,”alisema Barandagiye.
Kwa upande wao Shirika la
Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kupitia kwa Mwakilishi wao
nchini,Chansa Kapaya, wameahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania
kuhakikisha wakimbizi wa Burundi 6,800 walioomba kurejea nchini kwao
wanasahiliwa na kurejeshwa kwao katika hali ya utu na usalama huku
shirika hilo likizishukuru Serikali za Tanzania na Burundi kwa msaada
wao walioupata katika kushughulikia masuala ya wakimbizi.
No comments:
Post a Comment