Profesa Umanda, ambaye aliongozana na Afisa wa fedha wa shirikisho la wenye viwanda Tanzania,(CTI) Anna Kimaro ambaye kwa sasa anasoma katika chuo hicho, amesema uwekezaji
wa sekta ya viwanda ni moja ya njia ya kukuza uchumi wa nchi
kinachotakiwa kufanyika ni kuwa na viwanda vyenye nyenzo za teknolojia
ya kisasa na wataalamu ambavyo vinaweza kuzalisha bidhaa bora zinazoweza
kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Alisema
kuwa amefurahi kuona nchini Tanzania kuna kiwanda kikubwa kama TBL
ambacho kinafanya uzalishaji kwa kutumia mifumo na teknolojia za kisasa
sambamba na viwanda vilivyopo katika nchi zilizoendelea na kuongeza kuwa
uwekezaji katika sekta ya viwanda ukifanyika kwa umakini utawezesha
sera ya Tanzania kuelekea katika nchi ya viwanda kufanikiwa kwa haraka.
Akiongea na ujumbe huo,Afisa Mawasiliano wa TBL Group,Abigail Mutaboyerwa alieleza jinsi kampuni ya TBL Group mbali na kufanya uzalishaji kwa kutumia mifumo
na teknolojia za kisasa katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya
Mwanza,Arusha,Mbeya na Dar es Salaam inatekeleza sera ya ‘Dunia Maridhawa’ (Better world) ambayo imelenga kukuza viwanda sambamba
na kuboresha shughuli za utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na
kuboresha maisha ya watu kwenye jamii ambapo kampuni imewekeza.
“Sera
ya Dunia Maridhawa malengo yake yanashabihiana na malengo endelevu ya
Milenia ya Umoja wa mataifa (SDG’s) na sisi kama kampuni tunahakikisha
tunafanikisha malengo
haya na kwa kiasi kikubwa tumepata mafanikio hususani katika maeneo ya
kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira,matumizi mazuri ya maji
,kuendesha kampeni za utunzaji wa vyanzo vya maji,matumizi ya nishati
mbadala zisizo na athari kwa mazingira,kuharibu taka kwa kutumia
teknolojia za kisasa, na utakatishaji wa maji taka”.
Mutaboyerwa alisema katika kuhakikisha viwanda vya kampuni vinafanya uzalishaji bila athari kwa mazingira kampuni imeanza kutumia teknolojia mbadala zisizochafua hewa katika mchakato wa uzalishaji ambapo katika kiwanda cha TBL Mwanza kinafanya uzalishajinkwa kutumia pumba za mchele na katika kiwanda cha TBL Mbeya kimefunga mitambo ya kuzalisha umeme wa jua ambao utatumika katika shughuli za uzalishaji.
Aliongeza
kusema kuwa matarajio ya matumizi ya teknolojia mbadala za kuzalisha
nishati ya umeme ni kupunguza tani 130 za hewa chafu (Carbon Emmision)
kwa mwaka na kampuni inao mkakati kuhakikisha teknolojia hii inasambazwa
katika viwanda vyake vyote vilivyopo nchini na aliongeza kuwa kampuni yetu imefanikiwa kupunguza matumizi ya maji kutoka hectolita 6 ilizokuwa inatumia miaka ya karibuni hadi hectolita 3.6 kwa kila lita moja ya bia inayozalishwa.
Mbali
na mazingira alieleza mkakati wa kampuni wa kufanya kazi na wakulima
ambao wanaiuzia malighafi ambao umeanza kuleta mafanikio kwa
kuwanufaisha wakulima wa Shahiri wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro
sambamba na wakulima wa zabibu mkoani Dodoma. “Kupitia
mpango wetu wa kuwezesha wakulima maisha yao yamebadilika kuwa bora na
kupanua wigo wa ajira mashambani na tumejipanga kufanya kazi na wakulima wengi zaidi nchini lengo letu kubwa likiwa ni kuinua maisha yao,kuongeza kasi ya kukua uchumi na kujenga mfumo mzuri na endelevu wa kupata malighafi kwa ajili ya viwanda kampuni ya TBL Group kwa hapa nchini”.Alisisitiza.
Alimalizia kwa kusema kuwa TBL Group chini ya kampuni mama ya ABINBEV itahakikisha inashirikiana na serikali kufanikisha mkakati wa kujenga Tanzania ya viwanda na iko tayari kubadilishana uzoefu na taasisi mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi “Tunaamini tukishirikiana tutafanikiwa,ndio maana tumefungua milango kwa wageni kutoka taasisi mbalimbali ambao wamekuwa wakija kutembelea viwanda vyetu kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali”Alisisitiza
1.Profesa
Umanda kutoka Japan (kulia ) akibadilishana mawazo na Afisa Mawasiliano
wa TBL,Abigail Mutaboyerwa (katikati) na Anna Kimaro kutoka CTI kabla
ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda
Profesa
Umanda kutoka Japan (kulia ) akibadilishana mawazo na Afisa Mawasiliano
wa TBL,Abigail Mutaboyerwa (katikati) na Anna Kimaro kutoka CTI kabla
ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda
Profesa Umanda akipata maelezo kutoka kwa Mtalaam wa upishi wa bia wa TBL Group Christian Tarimo alipofanya ziara ya mafunzo kiwandani hapo
Mtaalamu wa masuala ya sera na uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Yamoguchi kilichopo nchini Japan, Tetsuji
Umada, amefanya ziara katika kiwanda cha bia cha TBL kilichopo Ilala
jijini ambapo alijionea shughuli za uzalishaji zinazoendeshwa na mifumo
ya kisasa na teknolojia za hali ya juu na kusema kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana na sekta ya viwanda inaweza kukuza uchumi wa Tanzania kwa haraka.
No comments:
Post a Comment