Jovina Bujulu-MAELEZO.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi za dunia hii imebabarikiwa kuwa na rasilimali
nyingi ambazo zikitumika ipasavyo itaondokana na tatizo la umaskini.
Hayo
yalibainishwa hivi karibuni na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.
Mbelwa Kairuki alipokuwa akizungumzia fursa za kibiashara zinazoweza
kupatikana nchini China na kuinua hali ya uchumi kwa wananchi wa
Tanzania.
Balozi
Kairuki alisema kuwa ni aibu kwa nchi za Kiafrika ambazo zimepata uhuru
kwa... zaidi ya miaka 50 kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi hususan nchini
China.
“Nchi
yetu imebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba, maji, mito na maziwa hivyo
tukitumia rasilimali hizi kwa kuunganisha na nguvukazi, uwezo na mitaji
tuliyo nayo tunaweza kabisa kupaisha uchumi wa nchi yetu sisi wenyewe”
alisema Balozi Kairuki.
Kwa
mujibu wa nyimbo za kujenga uzalendo kwa nchi zinakiri kuwa ni nchi
nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka, nasema kwa kinywa halafu
kwa kufikiri, nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania. Ni vema kuijenga
kuisimamia kwa manufaa ya Watanzania.
Balozi
Kairuki alisema kuwa kufuatia kusainiwa kwa mkataba kati ya Serikali ya
Tanzania na China, mwezi Mei mwaka huu watanzania watapata fursa ya
kuuza zao la muhogo mkavu nchini China kwa kiwango kikubwa hatua ambayo
itainua hali zao hilo kiuchumi na kuweza kuanzisha viwanda nchini.
“Hii
ni fursa, natoa rai kwa Watanzania wenzangu tuichangamkie na tujitokeze
kwenye maonesho ya biashara yatakayofanyika nchini China mwezi wa 10
mwaka huu, na kuhakikisha tunapata fursa ya kuona mashine za kuchakata
na kulimia ili tuweze kuzinunua na kuzitumia katika uzalishaji mazao ya
muhogo” alisema Balozi Kairuki.
Ili
kuhakikisha zao hilo linawanufaisha Watanzania, Balozi Kairuki alisema
kuwa ni muhimu kuchangamka fursa hiyo wasije wageni wakiwemo Wakenya na
Wachina wakaanza kulima zao hilo na kuwazidi Watanzania ambao ni
walengwa wa kupeleka zao hilo nchini China.
Aidha,
aliongeza kuwa kuwepo kwa fursa hiyo ni fahari kwa nchi Tanzania hatua
ambayo itatoa nafasi katika ngazi mbalimbali kununua mitambo ya
kuchakata mazao ya mihogo na kutengeneza bidhaa zitokanazo na muhogo.
Mkataba
huo utakuwa ni miaka mitano, Watanzania wanatakiwa kuchangamka mapema
ili kufaidi matunda ya uwepo wake kabla hujamalizika kwa namna
mbalimbali hata baada ya mkataba huo kuisha. Fursa hiyo inatoa nafasi
pia ya kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao yatokanayo na zao la muhogo
na hatimaye kukamata soko la bidhaa hiyo.
China
ni nchi ambayo ina mahitaji makubwa ya muhogo ambapo kwa mwaka
wanaingiza muhogo wa thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni
tano.
Katika
bara la Afrika nchi ya Nigeria ndiyo pekee inayouza muhogo China, hivyo
Tanzania itakuwa nchi ya pili barani Afrika kuuza muhogo nchini humo.
“Kutokana
na sababu za kijiografia Tanzania inaweza kusafirisha bidhaa hiyo kwa
urahisi zaidi kuliko nchi ya Nigeria hivyo ni rahisi kuteka soko la zao
hilo nchini China” alisema Balozi Kairuki.
Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inatakiwa kueleza taratibu za kufanya na
kutoa elimu kwa umma kuelezea taratibu za kufuata kuweza kulima muhogo
na kuuza nchini China.
Aidha,
wananchi wanatakiwa kulima kilimo chenye tija kwa kutumia teknolojia
ya kisasa ili kuzalisha mihogo yenye ubora na inayokidhi mahitaji ya
soko la kimataifa kwa wingi.
Balozi
Kairuki alitoa wito kwa wadau wa kilimo ambao ni pamoja na wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na taasisi zilizo chini yake, Halmashauri
na vituo vya utafiti wa kilimo kuwasaidia wakulima kutatua changamoto
zozote zinazoweza kujitokeza ili waweze kujipatia mazao mengi na
kuliteka soko la muhogo nchini China.
Nchi
nyingine ambazo zinazouza mazao ya muhogo nchini China ni pamoja na
Thailand, Brazil na Indonesia ambayo hutumika kutengeneza madawa,
biskuti na kwa ajili ya chakula.
No comments:
Post a Comment