Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na madereva
wa mabasi ya abiria pamoja na abiria wanaosubiri usafiri wa kwenda
mikoa mbalimbali na nchi jirani baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza
katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha
Ubungo, pamoja na kituo cha daladala cha Mbezi Luis
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimuelekeza Kamanda wa
Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Fortunatus Muslim kuhakikisha kuwa magari na mabasi yote ya
abiria yanakaguliwa mara kwa mara. IGP Sirro alifanya ukaguzi wa
kushtukiza jana katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi
jirani cha Ubungo na Kituo cha Daladala cha Mbezi Luis ( Picha na Jeshi
la Polisi)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ( katika) akiwa katika
ukaguzi wa kushtukiza kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi
jirani cha Ubungo, (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Kamanda wa Kanda maalum
ya Dar es salaam, Naibu Kamishna wa Polisi ( DCP) Lucas Mkondya
akifuatiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya
Dar es salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Awadhi Haji. ( Picha
na Jeshi la Polisi).
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro (katika) alipofanya ukaguzi
wa kushtukiza katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani
cha Ubungo na kituo cha daladala cha Mbezi Luisi, (kushoto) ni Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP) Murilo
Jumanne Murilo.
……………………………………………………………………………………..
Na Jeshi la Polisi
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka madereva na
wamiliki wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na
wamiliki na madereva wa mabasi madogo ya abiria maarufu kama daladala
kuhakikisha wanayafanyia ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara magari
yao ili kupunguza ajali zinazosababishwa na ubovu na uchakavu wa magari.
IGP
Sirro aliyasema hayo jana wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza
katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja
na kituo cha daladala cha Mbezi Luisi kwa lengo la kuangalia hali ya
usalama wa kituo hicho, kuona namna ukaguzi wa mabasi ya abiria
unavyofanyika kabla hayajaanza pamoja na kusikiliza kero mbalimbali
za abiria.
“Nimefarijika
kuona watendaji wa kituo hiki pamoja na askari wangu wakifanya kazi
vizuri kwa ushirikiano mkubwa hali inayosaidia kupunguza kero mbalimbali
kwa watumiaji wa kituo hiki” alisema IGP Sirro
Aliongeza
kuwa Ubungo ni salama na itaendelea kuwa salama kwa sababu vibaka
wamepungua na wale wanaofanya utapeli katika kituo hicho waache mara
moja na kutafuta kazi nyingine kwa kuwa mwisho wa siku wataacha familia
zao baada ya kukumbana na mkono wa sheria.
Pia
ameelekeza magari yote ya abiria yabandikwe namba simu zote za
makamanda wa mikoa wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Wakuu wa
Polisi wa wilaya zote sehemu ambazo itakuwa ni rahisi kuonekana na
abiria ili iwe rahisi kwao kutoa taarifa pindi wanapoona dereva
anaendesha gari kwa kukiuka sheria na kanuni za usalama barabarani.
Aliwataka
wananchi kuendelae kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa
taarifa za uhalifu na wahalifu ikiwa ni pamoja kutii sheria bila shuruti
na kutoa wito kwa wamiliki wa magari, madereva pamoja na abiria kuwa
wastaabu na kuhakikisha wanaheshimu sheria na kanuni za usalama
barabarani kwa kuwa kila mmoja anafahamu madhara ya ajali.
No comments:
Post a Comment