Mkurugenzi
wa mifuko ya Uwezeshaji toka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw.
Edwin Chrissant akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) fursa
zilizopo za uwekezaji kupitia mifuko ya hifadhi, katikati ni
Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi watoa huduma ya mafuta na
gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo.(Picha na
Eliphace Marwa – Maelezo)
Mkurugenzi
wa Taasisi ya sekta binafsi Dkt. Godfrey Simbeye akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu fursa mbalimbali zilizopo
katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Tanzania hadi Uganda, kulia
ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi watoa huduma ya mafuta na
gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana
Pallangyo (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka
Tanzania hadi Uganda, katikati ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa
Taasisi watoa huduma ya mafuta na gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim na
kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya sekta binafsi Dkt. Godfrey Simbeye.
Mwanzilishi
na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya watoa huduma ya mafuta na gesi
nchini Abdulsamad Abdulrahim akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba
la mafuta ghafi toka... Tanzania hadi Uganda, kulia ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya sekta binafsi Dkt. Godfrey Simbeye na kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Juliana Pallangyo.
………………………………………………………………….
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Wadau
wa Sekta ya Mafuta na Gesi wameshauriwa kujiunga na Jumuiya ya Watoa
Huduma wa Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS) ili waweze kunufaika na fursa
mbalimbali kwa urahisi.
Ushauri
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Mhandisi Dkt. Julia Pallangyo aliopokuwa
akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa Jumuiya hiyo.
Mhandisi
Dkt. Julia amesema kuwa Sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2015
inahamasisha ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Mafuta na Gesi
asilia hivyo uanzishwaji wa ATOGS umekua msaada mkubwa katika
utekelezaji wa Sera hiyo pamoja na kuimarisha ushiriki wa Watanzania
katika Sekta hiyo.
“Natoa
wito kwa watoa huduma kujiunga na ATAGOS kwa kuwa kufanya hivyo
kutawawezesha kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo ambao
utatoa fursa mbalimbali” Dkt. Julia alisema.
Alizitaja
fursa hizo kuwa ni pamoja na ujenzi, uhandisi, manunuzi na uwezeshaji
pamoja na huduma za kifedha na kibenki, huduma za bima, huduma kisheria,
ulinzi pamoja na chakula.
Kwa
upande mwingine, Naibu Katibu Mkuu amewakaribisha wananchi wa Tanga na
wa mikoa ya pembezoni kufika katika eneo la Chongoleani Jumamosi tarehe 5
Agosti mwaka huu kushuhudia uwekwaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa
bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania.
Akimuwakilisha
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji wa NEEC. Edwin Chrissant amesema kazi
moja wapo ya Baraza ni kusimamia, kuratibu na kufuatilia shughuli zote
za kiuchumi ikiwemo ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji hivyo mradi
wa ujenzi wa bomba la mafuta ni fursa kubwa ambayo Watanzania
wanaihitaji.
“Ujenzi
wa mradi huu ni moja ya miradi mikubwa kufanyika nchini ambao
utagharimu jumla ya shilingi trilioni 8 na bomba hili litakuwa na urefu
wa Kilomita 1445 kati ya hizo kilomita 1149 sawa na asilimia 80 ziko
Tanzania hivyo watanzania wakiwemo wale walio karibu na sehemu za ujenzi
huo wanahamasishwa kujiunga na ATOGS ili kujengewa uwezo wa jinsi ya
kutumia fursa hizo ”alisema Chrissant.
Chrissant
alifafanua kuwa bomba hilo ambalo litapita katika mikoa nane ikiwemo ya
Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara pamoja na
Tang,ujenzi wake utachukua kati ya miezi 24 hadi 36 hadi kukamilika.
Nae,
Makamu Mwenyekiti wa ATOGS, Abdulsamad Abdulrahim ameihakikishia
Serikali kuwa watoa huduma waliopo nchini wameonesha uwezo na utayari wa
kutoa huduma nyingi za kitaalam na nyinginezo zilizopo katika mnyororo
wa ongezeko la thamani zitakazohitajika wakati wa ujenzi wa bomba la
mafuta.
”Inatia
moyo kwamba ushiriki wa watoa huduma wa Tanzania katika Sekta hiyo
unapewa nguvu kisheria pia tunaishukuru Serikali ya Tanzania kwa
kuthibitisha msimamo wake wa kutaka kuona Watanzania wananufaika na
fursa za sekta hii jambo linaloleta matumaini mapya kwa jumuiya yetu,”
alisema Abdulrahim.
ATOGS
ilianzishwa kama chombo cha juu nchini kinachowakilisha na kusimamia
maslahi ya wadau na makampuni yanayotoa huduma katika sekta ya mafuta na
gesi nchini.
Uanzishwaji
wa Jumuiya hiyo ulizingatia uwepo wa fursa zitokanazo na rasilimali za
mafuta na gesi zikiwemo za ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta pamoja
na mipango iliyopo ya kusambaza gesi katika miji mikubwa nchini.
No comments:
Post a Comment