Mteja akipata huduma mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma,
|
Kampuni
inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania
imeendelea kuishi kulingana na ahadi yake ya kuwapatia wateja huduma
wanazozifikia kwa urahisi zaidi kwa huduma za Tigo kwa kufungua duka la...
huduma kwa wateja ambalo ni jipya lililofamnyiwa ukarabati mkubwa
leo katikati ya jiji la Dodoma .
Akizungumza
kwenye sherehe ya uzinduzi wa duka, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon
Karikari alisema duka iliyofanyiwa ukarabati ikiwa ni mkakati wa
upanuzi wa kampuni wa kuzileta bidhaa na huduma zake sehemu moja.
Duka
hilo jipya lililokarabatiwa miongoni mwa vitu vilivyomo ni pamoja na
sehemu ya watu mashuhuri (VIP) kwa ajili ya kuhudumia wateja ambao ni
VIP na wale wanaohitaji huduma za ufuatiliaji wa kasi, kaunta
zimeongezwa na eneo la kufanyia majaribio ambapo wateja wanaoingia
wanaweza kufurahia uzoefu wa kwanza wa kujifunza jinsi ya kutumia bidhaa
za Tigo kama vile simu za kisasa (smartphones) na bidhaa na huduma
nyingine za mtindo wa maisha ya kidijitali kama vile Tigo Pesa ambazo
zinatolewa na kampuni.
‘Tigo
imepania kutumia rasilimali zake zote ikatika kuhakikisha kuwa
wateja wetu wanapata huduma za daraja la juu duniani, kuhakikisha
ufanisi, wakati halisi wa majibu kwa maswali yao katika maduka yetu yote
52 ya huduma za wateja yaliyopo nchini, “alisema Karikari, na kuongeza
kuwa duka hilo mpya Iimewekwa vifaa vya kisasa, likihudumiwa na
wafanyakazi waliopata mafunzo sawasawa na ambao ni wachapa kazi ambao
wako tayari kutoa huduma bora kwa idadi ya watu inayoongezeka kwa
haraka jijini humo.
Akizungumza
juu ya uendeshaji wake, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George
Lugata alisema kuwa duka hilo jipya la Tigo mpya litakuwa wazi siku zote
saba za wiki.
“Kimkakati
kuwepo kwa duka hilo eneo la katikati ya jiji kunafanya iwe rahisi
kufikiwa na wakazi wa mji wa Dodoma, maeneo jirani na watu
wanaotembelea kitovu hicho cha nchi, ” aliongeza Lugata.
Aliendelea
kufafanua zaidi kuwa duka kubwa, la kisasa limekuwa pia linaenda bega
kwa bega na mkakati wa Tigo kupeleka huduma kwa wateja kwa wakazi wa
Dodoma kama mji ambao unatarajia kuwa ‘ mlipuko’ wa idadi ya watu
kufuatia uamuzi wa serikali kuhamishia shughuli zake za kiutawala
kutoka Dar es Salaam , na hivyo kufanya mji wa Dodoma makao makuu ya
nchi.
Duka
lipo mkabala na mzunguko wa CDA kwenye sakafu ya chini ya Jengo la CDA
Barabara ya Uhindini katika Manispaa ya Dodoma, na linatarajiwa
kuhudumia wateja zaidi ya 300 kwa siku.
|
No comments:
Post a Comment