Pages

Tuesday, August 1, 2017

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI NA WATENDAJI WAKE WAPITIA MPANGO WA MANUNUZI WA MWAKA WA FEDHA 2017/2018


Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Edward Peter Chogero akichangia hoja kwa Watendaji Wakuu, Maofisa Bajeti na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) wakati wa Kikao cha kupitia Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika leo Agpsti 1, 2017 katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi hilo. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akizungumza na Watendaji Wakuu, Maofisa Bajeti na Mipango wa Wizara yake wakati wa Kikao cha kupitia Mpango wa Manunuzi wa Wizara wa mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika leo Agosti 1, 2017 katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi hilo.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala, akifuatiwa na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa pamoja na Kamishna wa Polisi wa Fedha na Logistiki Albert Nyamuhanga.


Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi David Mwangosi, akiwasilisha Mpango wa Ununuzi wa Wizara hiyo wa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa Watendaji Wakuu, Maofisa Bajeti na Mipango wa Wizara hiyo wakati wa Kikao cha kupitia Mpango wa Manunuzi wa Wizara wa mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi hilo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa hiyo.



Kamishna wa Polisi wa Fedha na Logistiki Albert Nyamuhanga    akichangia hoja kwa Watendaji Wakuu, Maofisa Bajeti na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) wakati wa Kikao cha kupitia Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi hilo. Kulia ni Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa

No comments:

Post a Comment