Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ngao ya ushindi Bi. Zakia
Nassor Mkurugenzi wa Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited
ya jijini Dar es salaam kama ishara ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
ya Nje (TANTRADE) kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa udhamini wa
maonyesho ya baisaha yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya
Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Kulia anayeshuhudia ni Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimshuhudia Bi. Zakia Nassor
Mkurugenzi wa Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limitedi ya
jijini Dar es salaam wakati akimshukuru Mh. Waziri Charles Mwijage baada
ya kukabidhiwa ngao yake ya ushindi kama ishara ya Mamlaka ya Maendeleo
ya Biashara ya Nje (TANTRADE) kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa
udhamini wa maonyesho ya baisaha yanayoendelea kwa siku 14 kwenye
Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kutoka
kulia ni KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade), Edwin Rutageruka na Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE Bw. Christopher Chiza.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimshuhudia Bi. Zakia
Nassor Mkurugenzi wa Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited
ya jijini Dar es salaam wakati akishuka jukwaani baada ya kukabidhiwa
ngao yake ya ushindi kama ishara ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya
Nje TANTRADE kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa udhamini wa maonyesho
ya biashara yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya Sabasaba
Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade), Edwin
Rutageruka na Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE Bw. Christopher Chiza na
Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bi.
Zakia Nassor Mkurugenzi wa Utawala Kampuni ya Grobal Education Link
Limited wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye viwanja vya
maonyesho vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar essalaam leo.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka
kwa Bi. Zakia Nassor Mkurugenzi wa Utawala Kampuni ya Grobal
Education Link Limited wakati alipotembelea banda hilo leo kulia ni
Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage
Bi. Zakia Nassor Mkurugenzi wa Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited akizungumza na Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL aliyetembelea katika banda hilo, Kampuni ya Grobal Education Link Limited
imekuwa ikitoa ufadhili wa masomo kwa mhandisi mmoja wa shirika hilo
katika nchi ya China ambako amekwenda kuchukua ujuzu zaidi katika
uhandisi wa Ndege
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na msafara wake akiingia kwenye banda la Grobal Education Link Limited wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
………………………………………………………………………………………
Bi. Zakia Nassor Mkurugenzi wa
Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited ya jijini Dar es salaam
inayojishughulisha na kuwatafutia vyuo nje ya nchi wanafunzi wa
kitanzania amesema kampuni yake imewezesha wanafunzi kusoma kwa bidii
na wazazi kutopoteza fedha tena baada ya kuweka udhibiti kwa wanafunzi
wanaosoma nje ya nchi kupitia kampuni yao.
Bi. Zakia Nassor ameyasema hayo
wakati akizungumza na mtandao wa Fullshangwe kwenye maonyesho ya 41 ya
biashara yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje
(TANTRADE) na kufanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa
jijini Dar es salaam kila mwaka kuanzia Julai 1.
Amesema Kampuni yao inatoa
ushauri kwa wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma katika vyuo vya nje ikiwa
ni pamoja na kutoa ushauri kwa wazazi pia ili kujua watoto wao wanaweza
kusoma kozi gani kulingana na soko lililopo kwenye ajira ikiwa ni
pamoja na kujua viwango vya vyuo wanavyokwenda kusoma.
Ameongeza kwamba Kampuni hiyo
imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali kama vile TCU, NECTA na
NACTE ili kukidhi vigezo vya wanafunzi wenye sifa kujiunga na vyuo
hivyo katika suala zima la vyeti feki jambo ambalo linaokoa fedha
wanazotoa wazazi ili kulipia ada na kuwafanya wanafunzi wasome vyuo
hivyo huku wakiwa na uhakika na vyeti na taaluma zao mara watakapomaliza
vyuo na kurudi nyumbani tayari kuingia katika soko la ajira.
Kampuni hiyo imeweka utaratibu
mzuri wa kuhakikisha inawafuatilia wanafunzi katika mahudhurio na ufaulu
wa mitihani yao wawapo vyuoni ili kumrahisishia mzazi kufuatilia
maendeleo ya mtoto wake awapo chuoni ambapo kampuni hiyo imeweka
mawasiliano madhubuti na ya moja kwa moja na kati yake na vyuo
wanavyosoma watoto nje ya nchi ili kurahisisha wazazi kujua maendeleo ya
watoto wao.
Katika miaka ya hivi karibuni
kumekuwepo na wimbi la wanafunzi wengi kutomaliza masomo yao na
kujiingiza katika shughuli za biashara au kuacha masomo huku wazazi
wakiamini watoto wako shuleni. kumbe hakuna kinachoendelea, matokeo yake
wazazi wamekuwa wakipoteza fedha huku watoto wakishindwa kufikia
malengo kutokana na kufeli mitihani yao kwa sababu hakukuwa na
utaratibu wa kumfuatilia mwanafunzi akiwa chuoni
Kampuni hiyo imekuwa ikipeleka
wanafunzi wa kitanzania katika vyuo mbalimbali nje ya nchi ambavyo viko
katika nchi za Uingereza, Marekani, Canada, Australia, Ukrane, India,
Malaysia, China na Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment