Pages

Saturday, July 1, 2017

KAMPUNI YA PROPERTY INTERNATIONAL YACHUKUA USHINDI WA JUMLA KWA MAKAMPUNI YA UJENZI KATIKA MAONYESHO YA (TANTRADE) SABASABA

pr1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ngao ya ushindi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem ya jijini Dar es salaam kama ishara ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE) kutambua ushindi  wa kampuni hiyo kwa makampuni ya wajenzi na wauzaji wa vifaa vya ujenzi katika maonyesho ya biashara  yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Kulia wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya (TANTRADE) Bw. Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage
pr2 pr3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimnshuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem ya jijini Dar es salaam wakati akimshukuru Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage baada ya kupokea  ngao ua ushindi wa jumla kwa makampuni ya ujenzi na vifaa vya ujenzi  katika maonyesho ya biashara yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Kulia wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya (TANTRADE) Bw. Christopher Chiza.
pr4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimshuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem ya jijini Dar es salaam wakati akishuka jukwaani  mara baada ya kupokea  ngao ya ushindi wa jumla kwa makampuni ya ujenzi na vifaa vya ujenzi  katika maonyesho ya biashara yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kutoka Kulia wanaoshuhudia ni Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka na Mwenyekiti wa Bodi ya (TANTRADE) Bw. Christopher Chiza. Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage
pr5
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem kushoto  na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Masoud Alawi pamoja na mmoja wa maafisa wa kampuni hiyo wakionyesha ngao zao za ushindi.
pr6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akitembelea maonyesho hayo leo mara baada ya kuyafungua rasmi.
pr7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya kutembelea maonyesho hayo. hayo.
pr9
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem kulia akizungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw Ramadhan Kailima wakati alipotembelea katika banda la Kampuni ya Property International.
pr10
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem kushoto akizungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw Ramadhan Kailima wakati alipotembelea katika banda la Kampuni ya Property International katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Masoud Alawi.
pr11
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem kulia , Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima wa pili kutoka kulia  na, Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International  Bw. Masoud Alawi.
pr12
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem kulia na Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International  Bw. Masoud Alawi pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ushindi huo.
\pr13
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na ngao za ushindi.

No comments:

Post a Comment