Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokelewa
na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe mara baada ya kuwasili wilayani
humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Katikati ni Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana
na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Bw. Ahmed Shabiby mara baada ya kuwasili wilayani
humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe nawa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Gairo, Bi. Seriel Mchembe (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana
na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Cliford Tandari mara baada ya
kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimwagilia
mche alioupanda nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili
wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji
Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na
OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza
na viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo (hawapo pichani) katika mkutano
aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017 (Picha na OWM).
Viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo
wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika mkutano
aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017. (Picha na OWM).
No comments:
Post a Comment