Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka
shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
mara baada ya kuwasili Butiama ambapo atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe
za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akitoa heshima mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere mara baada kuweka shada la maua,Makamu wa Rais yupo Butiama kuhudhuria
sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani
Mara.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mkoa wa Mara mara baada ya
kuwasili Butiama kwenye makazi ya Hayati Baba wa Taifa.
NA MWANDISHI MAALUM, BUTIAMA
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili
mkoani Mara alasiri ya leo 3-June-2017 akitokea mkoani Mwanza ambapo
hapo kesho atakuwa ni mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.
Alipowasili
kijijini Butiama, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na
Viongozi wa vyama vya siasa na watendaji mbalimbali wa Serikali ambao
wameongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa pamoja na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba.
Makamu wa
Rais pia amepokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na amepata fursa ya
kuwasha mshumaa na kuweka shada la maua katika kaburi la baba wa Taifa Hayati
Julius Nyerere lililopo Mwitongo kijijini Butiama.
Hapo kesho tarehe 4-June-2017 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan ataongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Mara na mikoa ya Jirani katika
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo kitaifa sherehe hizo
zitafanyika katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment