BAADHI ya wanachama wa chama cha Mapinduzi
(CCM)wilayani Kibiti na Rufiji,mkoani Pwani ,wameutaka uongozi wa CCM
Taifa kuangalia namna ya kuahirisha uchaguzi wa chama kwenye wilaya hizo
ama mkoa kijumla .
Wameeleza hatua hiyo itawezesha wanachama kujipanga
kwa wakati mwingine ili
kupisha kadhia ya mpito ya vitendo vya mauaji
vinavyoendelea .
Aidha wamesema vitendo hivyo vinarudisha nyuma
maendeleo na uchumi wilayani humo na kukwamisha mipango ya kikanuni na
taratibu za vyama walizojipangia .
Hata hivyo ,wamesisitiza uwezekano wa vyama vya
siasa vikubwa wilayani hapo, kukaa kwa pamoja na wazee wa pande zote
kukemea vitendo hivyo.
Wakazi hao walibainisha kwamba,kwa umoja wao kutawezesha kushirikiana na serikali kumaliza janga hilo.
Muenezi wa Ccm wilaya ya Rufiji ,Musa Mnyelesa
,mkazi wa Kibiti Hadija Issa ,Hamis Kidongezo na Seif Mohammed
waliyasema hayo,baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kijiji na
mtendaji Wa kijiji cha Mangwi ,Mchukwi usiku wa kuamkia June 28 .
Walieleza ,hadi sasa hakuna uchaguzi uliofanyika wa
ngazi za chini ambako maeneo mengine unafanyika ,hakuna anaechukua fomu
ya kugombea .
Wanaongeza kuwa kila mwanachama anahaki ya kugombea na kupiga kura ili kuimarisha chama chochote kile .
Walisema kutokana na vitendo vinavyotia shaka na
kuonyesha Kibiti na Rufiji kutokuwa shwari ,ni vyema uchaguzi
ukaahirishwa ili baadae kupata haki za kichama wakiwa na amani .
Muenezi wa CCM Rufiji ,alisema chama mkoa na taifa wanapaswa kutupia macho suala hilo kwa upana kwa maslahi ya chama .
Mnyelesa alisema serikali na askari polisi wanafanyakazi nzuri lakini inabidi kujulikane kina cha tatizo.
“Naona kuna haja ya vyama vyote vikaguswa na hili
,maana hii agenda lisingekuwepo bunge ina maana viongozi wa vya vingine
vinavyokuwa na sauti kubwa ya kutetea mengi wasingeongeaa”
“Tunaomba wanasiasa ,viongozi wa dini ,wanaharakati
washikane mkono kuongeza juhudi za kupiga kelele kwa hili kama ilivyo
katika mambo mengine ya kijamii wanavyofanya” alisema Mnyelesa.
Mnyelesa alielezea kwamba ,bado wananchi ambao ni wanachama na viongozi wa CCM, vitongoji na vijiji wanaishi kwa hofu .
Nae Seif, alisema baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji wanashindwa kwenda ofisini kutekeleza majukumu yao.
Alisema wanaishi kwa sintofahamu na imani inawatoweka.
Anaeleza miaka ya nyuma watu walikuwa wakigombea
nafasi mbalimbali za uongozi lakini kwa sasa wanakwepa na kuhofia uhai
wao,na anahofu hata uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kuwa wengi
hawatajitokeza.
Hadija aliiomba serikali kuwadhibiti wahamiaji
haramu kwa kuwarudisha makwao badala ya kuachiwa kwani yawezekana
wakaleta athari kubwa ndani ya Mkoa na taifa kijumla .
Hadija alisema pia tatizo la wafugaji na wakulima liangaliwe kwani isije ikawa linachangia.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo, aliwaomba wananchi washirikiane na serikali kuwafichua wahalifu .
Ndikilo ,alieleza wauaji ama wahalifu wapo ndani ya
jamii hivyo endapo wananchi wataamua kuwataja watu hao itawasaidia
kuwakamata kirahisi.
Mkuu huyo wa Mkoa ,aliwataka kuwasema pia wageni kwenye maeneo yao kwani wageni wengine sio watu wema.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Onesmo Lyanga alibainisha kwamba,wanaendelea kupambana na kuimarisha ulinzi .
Ni matukio takriban 37 ya mauaji ya viongozi
mbalimbali wa chama, wenyeviti wa vijiji /vitongoji na askari polisi
ambayo yanadaiwa kujitokeza wilayani Rufiji ,Mkuranga na Kibiti,tangu
mwaka 2015.
Katika matukio hayo ni pamoja la March 28 ambapo
mwenyekiti wa (CCM) tawi la Mparange na mjumbe wa serikali ya kijiji
cha Ikwiriri Kaskazini ,Michael Lukanda,aliuawa kwa kupigwa risasi ya
kichwani .
Jingine ni march 12,mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo Hemed Njiwa aliuawa kwa kupigwa risasi.
Jan 19,mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.
March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana aliuawa.
Feb 24,watu watatu akiwemo afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Kibiti Peter Kubezya aliuawa kwa risasi.
April 13 mwaka huu,yalitokea mauaji ya askari polisi nane waliouawa kwa kupigwa risasi na wahalifu waliokuwa na silaha za moto .
Octoba 24,2016 afisa mtendaji wa kijiji cha Nyambunda Ally Milandu alipigwa risasi na kufa.
Novemba 6,2016 ,mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang’unda kijiji cha Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa risasi akielekea kwake.
Matukio mengine ni sanjali na May 17 ,mwenyekiti wa
CCM tawi la Njianne ,kijiji cha Muyuyu ,ambae pia ni mjumbe wa kamati
ya siasa kata ya Mtunda ,Iddi Kilungi ,aliuawa kwa kupigwa risasi.
May 13 mwaka huu,katibu wa CCM kata ya Bungu ,wilayani humo,Halife Mtulia ,kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
June 28 mwaka 2017 ,mtendaji wa kijiji cha
Mangwi,Shamte Makawa na mwenyekiti wa kijiji ,Hamis Mkima waliuawa na
nyumba tatu kuchomwa moto.
Na june 21 mwaka huu,askari Polisi wawili wa kikosi cha
usalama wa Barabarani wilayani Kibiti ,waligwa risasi na watu
wasiojulikana katika kijiji cha Msafiri .
No comments:
Post a Comment