Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Property International Bw. A. Haleem akishauriana jambo na Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo Bw. Masoud Alawi katika banda la kampuni hiyo lililoko
katika viwanja vya TANTRADE Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam
ambapo maonyesho ya biashara ya Sabasaba yanaendelea kuanzia jana na
yataendelea kwa muda wa siku kumi .
Kampuni hiyo inajishughulisha na
upimaji wa viwanja na kuuza kupitia mabenki mbalimbali ambayo wameingia
mkatataba nayo katika mpango huo mabenki yataweza kumlipia mteja wa
kiwanja kwa mkopo alafu mteja atarejesha rejesho kidogokidogo mpaka
atakapomaliza mkopo wake na kukabidhiwa hati ya kumiliki kiwanja chake
muhimu mteja atatakiwa kulipa asilimia 5 mpaka 20 mwanzo wa mkopo wake
kulingana na makubaliano ya kiwanja anachohitaji.
Kampuni hiyo pia
inajishughulisha na ujenzi wa nyumba na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya
ujenzi ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa visima vya maji, Katikati katika
picha ni Bw. Suleiman Abdallah Mchoraji wa ramani za majengo kutoka
kampuni ya Property International.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw.
Masoud Alawi akitoa maelezo kwa wateja waliotembelea katika banda hilo
leo ili kujionea mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na bidhaa
zinazopatikana katika banda hilo kulia ni Bw. Suleiman Abdallah Mchoraji
wa ramani za majengo kutoka kampuni ya Property International.
Bw. Suleiman Abdallah Mchoraji wa
ramani za majengo kutoka kampuni ya Property International akitoa
maelezo kwa Bw. Mahuna Tendwa kutoka Suma JKT aliyetembelea katika banda
la Property International katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw.
Masoud Alawi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Property International Bw. A. Haleem akishirikiana na mmoja wa
wafanyakazi wa kampuni hiyo kutoa maelezo na kuonyesha ramani za viwanja
vilivyopo jijini Dar es salaam na mkoa wa Pwani kwa wateja mbalimbali
waliotembelea banda hilo.
Mmoja wa wafanyakazi akiwa katika banda hilo ili kutoa huduma kwa wateja wanaotembelea katika maonyesho hayo.
Wateja wakiendelea kupata huduma katika banda hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa na nyuso za bashasha wakati wakikaribisha wateja katika banda ka kampuni hiyo.
Baadhi ya bidhaa zinazoonyeshwa katika banda hilo.
Bw. Abdul Msalam Mtaalam wa
masuala ya uchimbaji wa visima kutoka kampuni hiyo akiwa katika eneo
lake kama zinavyoo pampu mbalimbali maalum kwa ajili ya visima virefu na
vifupi.
Muonekano wa Banda la Property International linavyoonekana.
No comments:
Post a Comment