Rehema Mkamba Afisa Masoko
Mwandamizi LAPF akisoma wraka wa Matangazo ya vipindi kutoka kampuni ya
PPR iliyotembelea katika banda la mfuko huo lililopo kwenye Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
TANTRADE barabara ya Kirwa kwa lengo la kutangaza huduma zake katika
maonyesho ya 41 ya baiashara ya nje yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Bw. Juma Milinga Afisa Matekelezo
Mwandamizi LAPF akimpa maelezo Bw. Nungu Weswa mteja aliyetembelea
katika banda hilo ili kuionea huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko
huo.
Kulia ni Simboninsia Ndosi Afisa
Mafao LAPF na Sophia Matangalu Ofisa Mafao Mwandamizi LAPF wakiwa katika
maonyesho hayo ili kutoa maelezo mbalimbali kwa wateja wanaotembelea
kwenye banda hilo.
Afisa Matekelezo LAPF Bi. Agness
William akiwa tayari kwa kupokea wateja wanaotembelea katika banda hilo
wakati huu wa maonyesho ya sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADEBarabara
ya Kirwa jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa mfuko
huo wakitoa huduma kwa wateja mbalimbali waliotembelea katika banda la
LAPF kwenye viwanja vya Maonyesho vya TANTRADE Barabara ya Kirwa jijini
Dar es salaam, Kulia anayepata maelezo ni Cyprian Mpinda Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM.
Baadhi ya wafanyakazi wa LAPF wanaotoa huduma katika maonyesho hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Muonekano wa banda la LAPF.
No comments:
Post a Comment