Na MatukiodaimaBlog
WAKATI leo ni siku ya unywaji maziwa duniani kampuni ya maziwa ya
Asas Dairies Limited imenywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 4000 wa
shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa .
Shule
hizo za msingi zilizopo kanda ya Ruaha ambazo zimeanza kunufaika na
unywaji maziwa ,huku walimu wao wakidai baadhi ya wanafunzi wa
shule hizo wamekuwa na matokeo mabaya katika mitihani kutokana na
unywaji wa pombe ya kienyeji aina ya ulanzi
Meneja
wa miradi wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi alisema
kuwa maadhimisha ya mwaka huu yamelenga zaidi vijana hasa wanafunzi wa
shule za msingi mjini Iringa na ndio sababu kampuni yake imelazimika
kutoa msaada wa maziwa na majaketi kwa wanafunzi wanaotoka katika
familia duni .
Alisema
kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa iwapo shule zitaweka utaratibu wa kutoa
maziwa kwa wanafunzi afya za wanafunzi hao zitakuwa bora na kiwango cha
elimu kinaweza kuongezeka zaidi mashuleni.
Mbali
ya unywaji wa maziwa kuhamasishwa zaidi mashuleni bado viongozi wa
serikali wanapaswa kuanza kuhamasha unywaji wa maziwa katika ofisi hizo
za umma badala ya kutumia maziwa kutoka nje ya nchi .
Alisema kuwa kampuni ya Asas Dairies
Ltd
imeendelea kuunga mkono mpango wa lishe mashuleni kama njia ya
kuboresha afya na uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo Iringa unazalisha maziwa zaidi ya lita milioni 14 kwa mwaka ila bado kiwanda cha Asas kinasindika lita 400,000 pekee kwa siku .
Hata
hivyo alisema suala la lishe bado ni kikwazo katika mkoa wa Iringa
baada ya mkoa huo kuwa mkoa wa pili kwa utapiamlo kitaifa .
Hivyo alitaka jamii ya wakazi wa mkoa wa Iringa kujenga utamaduni wa kutumia maziwa ili kuongeza lishe na kuwa na afya njema.
Alisema
kuwa mkoa wa Iringa umejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa
maziwa mashuleni kwa kushirikisha wafugaji kama njia ya kukomesha
utapiamlo mkubwa mashuleni.
Kwani
alisema kuwa mkoa wa Iringa unapaswa kuondokana na aibu ya utapiamlo
kwa watoto na kuwataka wananchi sasa kuanza kuongeza ufugaji wa ng’ombe
za maziwa kupitia mradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe.
Hata
hivyo alipongeza jitihada za kampuni ya maziwa ya Asas kwa kuendelea
kuhamasisha unywaji wa maziwa na kuitaka jamii na mkoa wa Iringa
kuachana na unywaji wa pombe na badala yake kunywa maziwa zaidi.
Alisema kuwa mbali ya wanafunzi wa Manispaa ya Iringa kupewa
maziwa pia kampuni hiyo imeendesha zoezi kama hilo mkoani Kigoma .
Mwalimu mkuu msaidizi shule ya Msingi Ipogolo Makrina Mpogole
pamoja na kushukuru kampuni ya Asas kwa kutoa maziwa kwa wanafunzi
wote shuleni kwake bado alisema kampuni hiyo imetoa msaada wa
majacketi kwa wanafunzi wanaotoka familia zisizo na uwezo .
Mwalimu Mpogole alisema kuwa bado wanaomba wazazi kuangalia
uwezekano wa kuwawezesha watoto wao kupata japo paketi moja ya
maziwa fresh pindi wanapokwenda shule badala ya wanafunzi hao baadhi
yao kunywa pombe aina ya ulanzi .
Alisema matokeo mabovu kwa baadhi ya wanafunzi yanachangiwa na
tabia ya kunywa ulanzi wakiwa mitaaani hivyo iwapo watapewa maziwa
yatawasaidia kuongeza afya na kuwa na uwezo zaidi katika masomo .
Wakati mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi JJ Mungai Haji
Mpakati alisema kuwa iwapo utaratibu wa wanafunzi kupewa lishe
unaweza kupunguza kiwango cha udumavu na utapiamlo kwa wanafunzi
mashule.TAZAMA VIDEO HAPA CHINI |
No comments:
Post a Comment