Akizungumza kwenye uzinduzi wa
mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela alisema
mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi hao kwani yatawasaidia kupata mbinu
mpya ambazo watazitumia wakati wa kutengeneza mipango mikakati katika
maeneo yao.
Alisema kwa dhamana waliyonayo
watumishi hao ni vyema kutumia mafunzo hayo ya siku mbili vizuri ili
baada ya mafunzo waweze kupata njia mbadala katika uandaaji wa mipango
mikakati ambayo itasaidia kuleta maendeleo
“Hampo hapa kwa ajali, mpo
kwasababu dhamana zenu ni kubwa, kwa kupitia mafunzo haya mtapata nyezo
za kupangia mikakati ya kweli na mimi nataraji mtatoka hapa vizuri, haya
ni mafunzo muhimu sana,
“Tusiishie kwenye mikakati, tatizo
ni jinsi gani ya kuanzisha miradi, tumekuwa na mawazo mengi sana lakini
tuna changamoto ya kuyaweka kwenye miradi, tutoke kwenye kuwa na mawazo
na sasa tuanze kuyafanyia kazi,” alisema Mongela.
Pia Mongela aliwashukuru ESRF kwa
kuandaa mafunzo hayo na kuwataka washiriki kufanya kazi kwa ushirikiano
na ESRF kwani tayari wameonyesha nia ya kushirikiana nao ili kuhakikisha
mipango ambayo wanaipanga inafanyiwa kazi.
“Tuone jinsi gani tunatumia fursa
hii vizuri, tunatakiwa tukitoka hapa tukatekeleze mipango hii na ESRF
wapo tayari kushikana mikono na sisi hadi waoane mafanikio na mimi
niwahakikishie sisi tupo tayari … nategemea mambo makubwa baada ya
kuanzisha ushirikiano huu,” alisema Mheshimiwa Mongela.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF,
Dk. Tausi Kida alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa mstali wa mbele
kusukuma mbele Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa kufanya shughuli
mbalimbali ambazo zinakuwa muhimu kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa
ujumla.
“Kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali, wa nje na ndani ya nchi, ESRF imekuwa ikisimamia na kuhimiza
ufikiwaji wa malengo hayo sio tu katika ngazi ya Taifa bali pia katika
ngazi ya wilaya na hata Kata,” alisema Dk. Kida
Dk. Kida aliendelea kusema kuwa
mafunzo hayo kutakuwa na mada zinazoelezea maelezo ya Jumla kuhusu
mpango mkakati, upangaji wa bajeti, ufuatiliaji na namna ya kutoa
taarifa, mikakati ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa SDGs, FYDP II,
Africa Agenda 2063, Vision 2025, mchakato wa kuandaa mpango mkakati na
ufuatiliaji, upimaji, na utoaji wa taarifa (reporting, monitoring and
evaluation)
Aidha ESRF imezindua mwongozo wa
kuandaa mipango mkakati ya wilaya, mwongozo ambao umetokana na andiko
kubwa lililoandaliwa na serikali siku za nyuma kuhusu uandaaji wa
mipango mkakati ya muda wa kati pamoja na bajeti (Government’s Medium
Term Strategic Planning and Budgeting Manual).
No comments:
Post a Comment