Pages

Thursday, June 1, 2017

BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Mwenyekiti wa Baraza la wazee mkoa wa Arusha
Mathius Kichao aliyeshika karatasi
mkononi,akiwa anazungumza na waandishi wa habari hivi katibuni Jijini
hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu
wa wazee wa Baraza la wazee Jijini Arusha
Kassim
Seremuka
  akizungumza jinsi ambavyo wazee hao
wamenifaika na vitambulisho vya bima ya afya
.Picha
na Vero Ignatus Blog.
 
Baadhi
ya viongozi na wajumbe wa Baraza la wazee katika mkoa wa Arusha wakiwa
katika picha ya pamoja .Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu
wa Baraza la wazee
Kassim Seremuka Jiji
la Arusha akionyesha Kadi ya matibabu wanazotumia wazee wakienda
kutibi wa Hospitalini
.
Na.Vero Ignatus, Arusha.
 Baraza la Wazee Jijini Arusha
wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli
kuwaangalia wazee ambao walikuwa  Jumuiya ya Afrika

Mashariki awalipe  stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii mambo
mazuri bali manufaa wameyakosa baada ya kuvunjika Jumuiya
hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari  kwa niaba ya
wazee hao mwenyekiti wa Baraza hilo 
Mathius
Kichao
amesema  kuwa hadi sasa kuna wazee ambao
hawajalipwa stahiki zao jambo ambalo siyo zuri hata kidogo kwani wazee
hao wananung’unika
  “Kuna
muda wazee hawa waliandamana wakenda Dar es salaam ,wakalala
barabarani,lakini viongozi wawakati ule hawakuona umuhimu kuwa kilio cha
wazee ni hatari sana wakawafukuzwa,nitamke kuwa hadi sasa kuna wazee wa
jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa chochote kile,
niikumbushe
Serikali wale
wazee wanalaani ,naomba hii laana
isitokee,Mhe,Magufuli awalipe stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii
vizuri zaidi 
“alisema Mwenyekiti huyo



 Aidha wazee hao  katika jiji la Arusha
wameiomba serikali ya awamu ya tano ipeleke  mswada wa wazee
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano  na upitishwe  ili
Wazee nchini Tanzania  waweze kunufaika na matunda ya nchi yao
kwani  wao ni chombo cha harakati hivyo Taifa likiwasahau wazee
hakuna maendeleo kwasababu  wazee  huwa  wanafahamu
mambo mengi ya kihistotia ya Nchi pamoja na mila nzuri na
desturi.
“Tunawaomba viongozi mbalimbali wa Taifa hili
wanapotembelea mkoa wa Arusha watenge muda wao ili waweze kuonana na
wazee tutawashauri kwa yale tunayoyafahamu kwaajili ya manufaa ya nchi
yetu na watoto pamoja na wajukuu zetu.
Katibu wa
wawazee katika Jiji la Arusha Kassim Seremuka amesema
kuwa  baada  ya Taifa kupata uhuru 1961 serikali ilianza
kuweka katika ajenda zake maswala yanayohusu wazee,ambapo mwaka 2002
umoja wa Mataifa wakapitisha maazimiao yake ambapo Tanzania kama nchi
iliyasaini  kuhusiana na haki za wazee ndipo kuanzia hapo ndipo
serikali  ikaandika Sera ya Taifa ya Wazee.
Amesema
kuwa katika  Sera hiyo iliainisha mambo mengi ikiwemo haki ya
msingi ya kikatiba,za kisheria haki za msingi za kibinadamu,ambapo
serikali iliweka matamko kuwa  katika ibara ya2( 2,1) inasema
sera hiyo inawahusu wazee waliopo vijijini na mjini ,pamoja na makundi
maalumu ya wazee wakiwemo wastaafu,wakulima ,wafugaji,na wavuvi
,amesema sera hiyo inawahusu vijana wanaofanya maandalizi ya uzee
mwema .
Amesema
kuwa wao kama baraza la wazee jiji la Arusha limesaidia wazee
kutambulika ndani ya miezi 7 kuanzia mwezi wa 10 2016 wameweza
kuwaratibu na kuwaandikisha kwaajili ya vitambullisho vya bima ya afya
tayari wazee zaidi ya 6000 wameshapata vitambulisho hivyo kwa
kusaidiwa na halmashauri ya jiji imetoa sh milioni kumi na mbili
kwaajili ya mpango wa Tiba kwa kadi (TIKA)
Katibu
huyo amesema kuwa fedha hizo imegawanywa kwenye vituo vya afya,vya
kata na halmashauri,amesema wazee wakienda hospitali wanakwenda na
kadi zao na wanatibiwa hadi kwenye hospitali ya rufaa ya mount Meru
bila kipingamizi chochote .


No comments:

Post a Comment