Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Dkt.
Dkt. Alexander Kyaruzi akitoa maelekezo wakati wa kuikabidhi rasmi
majukumu bodi mpya ya TGDC.
Matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Bodi ya TGDC.
……………………………………………..
Na Johary Kachwamba -TGDC
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Umeme nchini (TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi amezindua rasmi Bodi mpya
ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi nchini (TGDC) na
kuipa vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu. TGDC ni kampuni tanzu ya
TANESCO
Uzinduzi wa Bodi hiyo ulifanyika
jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Ofisi za TGDC na kuhudhuriwa
na wajumbe wa menejimenti ya kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
bodi hiyo Dkt. Kyaruzi alisema kulingana na majukumu ya TGDC waliona ni
vyema wachague Wakurugenzi wenye taaluma tofauti ili kuisaidia kampuni
katika nyanja mbalimbali.
“Tuliona kwa shughuli za uendelezaji geothermal
basi tutafute mtaalam wa jioloiia, tukamteua Dkt. Mshiu, Uhandisi Dkt.
Mwinuka na mtaalam wa mambo ya fedha Ndugu. Segeja” alisema Dkt.
Kyaruzi.
Akizungumza Kaimu Meneja Mkuu wa
TGDC, Mhandisi. Kato Kabaka alimshukuru Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya
TANESCO kwa uteuzi huo, na kuahidi kuipatia Bodi ushirikiano kwa
kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu.
Naye Mwenyekiti mteule wa Bodi ya
TGDC, Ndugu. Beatus Segeja alieleza watashirikiana vyema kwa kutumia
taaluma zao kutimiza majukumu waliyokabidhiwa ya kuisimamia TGDC.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ya
Wakurugenzi wa TGDC, Ndugu, Beatus Segeja anaongoza wajumbe wengine
wawili ambao ni Dkt. Tito Mwinuka na Dkt. Elisante Mshiu.
No comments:
Post a Comment