Meneja Mawasiliano na Masoko wa
kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Cletus Mnzava akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu
uimarishaji wa Ofisi za Kanda ili kusogeza huduma karibu na
wananchi.kushoto ni Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bw. Sylivesta Omari.
Meneja ukaguzi wa Kemikali Bw.
Fidelis Segumba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini
Dar es Salaam.kulia ni Meneja Mawasiliano na Masoko wa Ofisi ya Mkemia
Mkuu wa Serikali Bw. Cletus Mnzava
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali
imedhamiria kuimarisha Ofisi za Kanda ili kusogeza huduma kwa wananchi
katika Mikoa yote ,ikiwa ni katika juhudi zake za kuimarisha utendaji na
kuongeza tija na uwajibikaji.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano na Masoko wa Ofisi hiyo Bw. Cletus
Mnzava ,alipozungumza na waandishi wa habari juu ya majukumu ya Ofisi
hiyo na huduma zinazotolewa.
“Mwelekeo ni kuimarisha Ofisi
zetu za Kanda ili kusogeza huduma karibu kwa wananchi, kwa sasa
tunaendelea kuimarisha Ofisi ya Dodoma kama Makao Makuu ya Nchi ambayo
pia
itahudumia Mikoa ya Iringa,Morogoro na Singida” Alisisitiza Mnzava.
Akifafanua Mnzava alisema Ofisi
hiyo imejipanga kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga
Tanzania ya Viwanda kwa sababu viwanda vitakuwepo kila kona ya nchi na
viwanda vinatumia kemikali hivyo vinatakiwa vifuatiliwe kwa ukaribu ili
matumizi yafanyike kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizowekwa.
Aliongeza kuwa moja ya mikakati
ya Ofisi hiyo ni kuwepo kwa watumishi wanaodhibiti uingizwaji wa
kemikali usiofuata taratibu ambapo wakaguzi hao kwa sasa wako katika
mipaka ya Namanga,Holili na Horohoro kwa upande wa kanda ya Kaskazini.
Kwa upande wa Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini wakaguzi hao wako katika mipaka ya Tunduma,Kasumulu na
Mutukula ,Sirari kwa upande wa Kanda ya Ziwa ambapo mpango mkakati wa
Ofisi hiyo ni kuhakikisha kuwa Lengo la Serikali kusogeza huduma karibu
na wananchi linatimia.
Kwa upande wake Meneja wa Ukaguzi
wa Kemikali Bw. Fidelis Segumba amesema Maabara hiyo imejipanga
kuwahudumia wananchi vizuri nyakati zote.
No comments:
Post a Comment