Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati Wafanyakazi wa
Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi wakiwa wanapita mbele yake kwa
njia ya maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo nchini
yamefanyika Kitaifa katika Chuo cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista
Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki
pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)
Tumaini Nyamhokya.
Sehemu ya Wafanyakazi waliofika
kwenye Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika
mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono wakati wa
wimbo wa Mshikamano daima pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista
Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki,
Rais wa Shirikisho la Vyama vya vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini
Nyamhokya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Saidik.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amenyanyua juu mikono mara baada
ya kuimba wimbo wa Mshikamano Daima pamoja na Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye
ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora
Angela Kairuki Rais wa Shirikisho la Vyama vya vya Wafanyakazi Tanzania
(TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said
Meck Saidik.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akitoa salamu za Mkoa kwenye Sikukuu hiyo ya Wafanyakazi Duniani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akitoa
salamu katika Sikukuu ya Wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya akizungumza katika
Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani
Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika
kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika
Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi na wadau
mbalimbali waliohudhuria katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi
Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha
Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakazi wawili wenye
ulemavu mara baada ya kumaliza kuhutubia katika kilele cha Sikukuu ya
Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa
Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Wafanyakazi mbalimbali
wakati akiondoka katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi mara baada ya
kuhutubia katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani. PICHA NA
IKULU
No comments:
Post a Comment