MITI
mbali mbali ikiwa imeanguka katika moja ya sehemu ya Barabara ya
Chake-Mkoani, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA) Kwa hisani ya ZanziNews
MAGUNIA
518 ya Karafuu Kavu zikiwa hazikuharibika katika ghala la kuhifadhia
karafuu la Shirika la ZSTC Mkoani, baada ya ghala hilo kuanguka sehemu
ya Ukuta na gunia tisa kufukiwa na dongo zikiwa na karafuu kavu.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
SEHEMU ya
Ghala la Kuhifadhia karafuu la ZSTC Mkoani, likiwa limebomoka baada ya
kuangukiwa na mti uliokuwa katika mlima na kupelekea Gunia Tisa za
Karafuu Kavu zenye thamani ya Zaidi ya Milioni 5 kufukiwa na dongo
kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
WATOTO
wadogo wakisafisha kwa kutoa dongo nje katika Msikiti wa Mbuyuni Wilaya
ya Mkoani, baada ya sehemu kubwa ya msiki huo kuangukiwa na Udongo
ulioporomoka na kuharibu Msikiti, kama unavyoonekana katika Picha.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WATOTO
wadogo wakisafisha kwa kutoa dongo nje katika Msikiti wa Mbuyuni Wilaya
ya Mkoani, baada ya sehemu kubwa ya msiki huo kuangukiwa na Udogo
ulioporomoka na kuharibu Msikiti, kama unavyoonekana katika Picha.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WANANCHI
wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, wakitoa msaada kwa kuondosha Udongo, ili
kutoa Vitu vilivyofukiwa na Fusi baada ya Nyumba ya Fadhil Amour Mohamed
kuangukiwa na Udongo na kutokupata hata kitu Kimoja.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
SOMA ZAIDI »
No comments:
Post a Comment