Pages

Monday, May 1, 2017

JAMII YATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UPIMAJI WA ARDHI.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimkabidhi mkazi wa Lamadi, Mama Juma hati miliki ya eneo lake.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Lamadi juu ya kuwa na hati miliki ya maeneo yao
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akifurahia jambo na wakazi wa Lamadi.

Na Shushu Joel,BUSEGA.

JAMII imetakiwa kuchangamkia fursa zinazoendelea kutolewa na serikali katika ufanikishaji wa wananchi wote kupima maeneo yao ili waweze kuwa wamiliki halali kwa kupatwa hati za kumiliki maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya nyumba ya Makazi, Mh William Lukuvi alipokuwa akikabidhi hati halali za umiliki wa maeneo kwa wakazi wa kata ya lamadi,wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Unapopimiwa eneo lako unakuwa na faida nalo kubwa sana ambalo kwa sasa ni vigumu kuiona na hii ni kutokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya uthamani ya kumiliki wa hati ya eneo.

“Unapokuwa na hati ya kiwanja chako au nyumba yako unakuwa na thamani kubwa na hii ni kutokana na kuwa unaweza ukauaga umasikini kwa kukopesheka na mabenki mbalimbali na hivyo kuwa na mtaji wa kufanya biashara zako bila kuwa na usumbufu wa aina yeyote ile” alisema Mh Lukuvi.

No comments:

Post a Comment